YANGA YATUA MBEYA, KUKIPIGA LEO HII
Kikosi cha Yanga kimewasili jijini Mbeya asubuhi ya leo kwa kwa ajili ya mchezo wao wa raundi ya tatu ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) dhidi ya Ihefu FC.
Yanga iliondoka asubuhi ya leo kwa ndege kutoka Dar es Salaam ambapo ni saa chache kabla ya mchezo huo ambao utachezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini hapo.
Mchezo huo utachezwa leo saa kumi jioni.
Comments
Post a Comment