KAGERA SUGAR 0-2 SIMBA ‘LIVE’ UWANJA WA KAITABA


Mwamuzi anamaliza mchezo, Simba ikiwa ugenini inapata ushindi wa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Kaitaba, wafungaji ni Said Ndemla na John Bocco.
Dakika ya 94: Okwi anakosa nafasi ya wazi hapa, kipa Juma Kasena anafanya kazi nzuri ya kuudaka mpira
Dakika ya 90: Zimeshaongezeka dakika mbili, Simba wanapata kona.
Dakika ya 89: Mashabiki wa Simba wanaongeza shangwe.
Dakika ya 86: Straika wa Simba, Laudit Mavugo anapasha misuli, nje.
Dakika ya 83: Mchezo umechangamka, kasi imeongezeka, Kagera wanafunguka, Simba nao wanapanda kushambulia.
Dakika ya 79: John Bocco anaipatia Simba bao la pili akimalizia pasi nzuri ya Shomari Kapombe.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dakika ya 74: Kagera wanapata faulo, inapigwa vizuri lakini Manula anadaka.
Shangwe za Simba zinaongezeka.
Dakika ya 70: Shomari Kapombe wa Simba anaingia, anatoka Gyan.
Dakika ya 69: Said Ndemla anaipatia Simba bao la kwanza kwa shuti kali.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dakika ya 65: Mchezo umebalansi, timu zote zinashambuliana kwa zamu.
Dakika ya 60: Kagera wanafanya mabadiliko, anatoka Patory Athanas, anaingia Edward Christopher.
Dakika ya 53: Beki wa Simba, Juuko Murshidi anapewa kadi ya njano kwa kucheza vibaya.
Dakika ya 48: Kagera wanaonekana kuwa makini na kujilinda vizuri.
Kipindi cha pili kimeanza
MAPUMZIKO
Dakika ya 47: Kipindi cha kwanza kimekamilika.
Zinaongezwa dakika mbili za nyongeza.
Dakika ya 45: Simba wanarudi nyuma kujipanga, wanaanzisha mashambulizi kutokea nyuma.
Dakika ya 40: Nahodha wa Simba, John Bocco anapewa kadi ya njano.
Dakika ya 35: Simba wanapata faulo.
Dakika ya 34: Beki wa Kagera Mohamed Fakhi anapata kadi ya njano kwa kucheza faulo.
Dakika ya 27: Mpira unachezwa katikati ya uwanja muda mwingi.
Dakika ya 25: Simba wanalikabili lango la Kagera Sugar lakini umakini unakuwa mdogo, mpira unatoka nje.
Dakika ya 18: Simba wanapata faulo nje ya 18 ya Kagera Sugar.
Dakika ya 15: Simba wanapata kona. Inapigwa inaokolewa.
Dakika ya 8: Timu zote zimeanza kwa kasi ndogo. Beki wa Kagera, Juma Nyosso anapewa kadi ya njano kwa kumzonga mwamuzi.
Dakika ya 5: Wachezaji wa Kagera Sugar wanamzonga mwamuzi, lakini refa anakuwa mkali.
Dakika ya 6: Timu zote zimeanza kwa kasi ya kawaida.
Mwamuzi anaanzisha mchezo.
Hiki ni kipute cha Ligi Kuu ya Vodacom kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera Sugar ni wenyeji wanakutana na Simba kutoka Dar es Salaam.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!