Posts

Showing posts from August, 2019

Zahera afumua kikosi chote Yanga

Image
Kikosi cha yanga kilichofungwa na Polisi Tanzania KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera ameamua kufumua kikosi chote huku akisisitiza kwamba hafanyi mambo kufurahisha mashabiki. Zahera amekwenda mbali na kusisitiza kwamba hata katika mechi ya kirafiki leo Jumapili dhidi ya AFC Leopards hakuna hata mchezaji mmoja aliyecheza Moshi dhidi ya Polisi Tanzania atakayeanza. Katika mechi dhidi ya Polisi juzi Ijumaa Yanga ilifungwa mabao 2-0 huku ikianzisha sura nyingi mpya. Zahera amekwenda mbali zaidi kwa kusema kwamba hata kwenye mechi ya marudiano dhidi ya Township Rollers hakuna mchezaji yoyote aliyecheza dhidi ya Polisi ataanza. Kikosi cha kwanza kilichoanza dhidi ya Polisi kilikuwa na Ramadhani Kabwili,Mustafa Seleman,Gustava Saimon,Ally Ally,Kelvin Yondani,Abdulaziz Makame,Maybin Kalengo,Feisal Salum,David Molinga na Deus Kaseke. Kocha huyo anayezungumzia Kiswahili cha lafudhi ya Kicongo amesisitiza kwamba anakifanyia mabadiliko makubwa kikosi hicho ili kupata ubora ana

La Galaxy Wampa Ninja Namba 51

Image
 BEKI wa zamani wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ juzi Ijumaa alitambulishwa rasmi katika mtandao wa klabu ya La Galaxy II kama mchezaji wa timu hiyo huku akiwa amepewa jezi namba 51. Ninja amejiunga na timu kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea katika timu ya MFK Vyskov ya Jamhuri ya Czech baada ya kumaliza mkataba wake wa miwili na Yanga akiwa ametokea Taifa Jang’ombe ya Zanzibar. Ninja alitambulishwa katika mtandao rasmi wa timu hiyo ambao unahusika kutoa taarifa za timu hiyo anayocheza mshambuliaji wa zamani wa Barcelona na Manchester United, Zlatan Ibrahimović. Akizungumza na mtandao huo, meneja mkuu wa timu hiyo, Dennis te Kloese alisema kuwa wamesaini beki huyo kutoka Tanzania kwa mkataba wa mkopo wa muda mrefu akitokea katika klabu ya MFK Vyskov huku akiwa tayari ameshapa kibali chake cha uhamisho wa kimataifa ITC na kibali cha kufanyia kazi nchini maarufu kama P1 Visa. “Tumemsajili Abdalla (Ninja) katika orodha ya wachezaji wetu kwa ajili msimu ujao wa

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

Image
 NAHODHA wa timu ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’, Mbwana Samatta amefunga mabao matatu (hat-trick), katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza nchini Ubelgiji dhidi ya Waasland-Beveren. Samatta aliiongoza klabu ya KRC Genk kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 katika mchezo huo uliochezwa juzi, kwenye Uwanja wa Freethielstadion, mjini Beveren. Mshambuliaji huyo alifunga mabao hayo, dakika za 53, 66 na 86, huku bao jingine likifungwa na Joseph Paintsil dakika ya 21. Samatta anakuwa mshambuliaji wa tatu kufikisha mabao manne, baada ya kucheza michezo minne ya ligi hiyo msimu huu, wengine ni Dieumerci Mbokani wa Royal Antwerp na David Okereke wa Club Brugge. Huo ni mwanzo mzuri kwa Samatta ambaye msimu uliopita aliimaliza nafasi ya pili kwenye chati ya wafungaji bora wa ligi hiyo , akiwa na mabao 23, mabao mawili nyuma ya Hamdi Harbaoui wa Zulte Waregem aliyechukua kiatu cha ufungaji bora. Samatta sasa amefikisha mabao 66, katika mechi ya 160 za mashindano yote, tangu

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!

Image
 ACHANA na mechi ya Man city na Spurs, ngoma leo saa 1 usiku iko kwenye Uwanja wa Taifa kwa Simba na azam. Kwa lugha rahisi ni kwamba wenye mpira wao Tanzania wanafungua msimu mpya kwa burudani ya Ngao ya Jamii. Kuanzia nje mpaka ndani ya Uwanja hizi ndizo klabu zenye bajeti kubwa zaidi na leo zinakutana Taifa kuonyeshana ubabe na kufungua njia mpya. Ni mechi ngumu na itakayokuwa na utamu wa aina yake. Ni lazima mtu akae, hakuna cha sare wala suluhu. Mtaalam Razack Abalora atasimama kwenye lango la Azam huku pembeni katika ulinzi wakisimama Nicholas Wadada na Bruce Kangwa. Pale kati atakuwepo Daniel Amoah na Oscar Masai. Kati yupo Yakub Mohammed, Abdallah Masoud, Salmin Hoza, Salum Aboubakary ‘Sure Boy’ na Idd Seleman. Huyu ni wakuitwa Nado. Pale mbele anamalizia Obrey Chirwa mwenyewe. Simba sasa. Aishi Manula hayuko fiti. Beno Kakolanya ataanza chini ya ulinzi wa Shomari Kapombe,Hussein Mohammed ‘Tshabalala’, Pascal Wawa na Tairone Dos Santos. Kuna mtu anai

Passport Yamuondoa Balama

Image
 IDARA ya Uhamiaji Tanzania imemzuia kiungo mshambuliaji mpya wa Yanga, Mapinduzi Balama kujiunga na kambi ya kujiandaa na mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Yanga imeingia kambini Jumanne ya wiki hii huko Chuo cha Mwika Wildlife kilichopo Moshi, Kilimanjaro ambako inajiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Township Rollers ya Botswana. Timu hizo zinatarajiwa kucheza mchezo huo wa marudiano Agosti 24, mwaka huko Botswana baada ya awali kutoka sare ya kufungana bao 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar. Mratibu wa timu hiyo, Hafidh Saleh amesema kuwa, kiungo huyo aliachwa Dar kwa ajili kukamilisha kibali cha kusafiria kinachosimamiwa na Idara ya Uhamiaji. “Balama yupo njiani, hapa ninavyozungumza na wewe, tulishindwa kuja naye ili akamilishe hati yake ya kusafiria. “Ilikuwa lazima tumuache Dar ili ajiunge na wenzake baada ya kocha kuutaka uongozi ukamilishe haraka hati yake ya kusafiria tayari kwa safari ya Botswana. “Hivyo, Balama yupo nj

Rage: Kwa Deo Kanda, Kahata Simba SC Imelamba Dume

Image
 ISMAIL Aden Rage ambaye ni mwenyekiti wa zamani wa Simba, ameweka wazi kuwa timu hiyo imelamba dume kwa kuwasajili mshambuliaji Deo Kanda na kiungo Francis Kahata. Deo Kanda amejiunga na Simba kwenye usajili huu mkubwa kwa mkopo kutoka TP Mazembe na Kahata amesaini miaka miwili akitokea Gor Mahia ya Kenya. Akizungumza na championi Jumamosi, Rage alisema kuwa Kahata na Deo Kanda ni kati ya usajili bora ambao Simba wameufanya na anaamini watakuja kusumbua sana msimu ujao. “Simba imefanya usajili mzuri, ukiangalia walicheza mechi ya kirafiki na wachezaji wale wachezaji wapya, Deo Kanda na Francis Kahata wakikaa vizuri watasumbua sana pale Simba, kwa ubora wa na hilo halina ubishi. “Yaani namna wanavyocheza unaona kabisa hapa kuna kitu ndani yao hivyo wakitumiwa vyema watakuwa msaada kwenye timu hiyo katika mashindano tofauti,” alisema Rage na kuongeza: “Pia kuna Shomary Kapombe aliyekuwa majeruhi naye amerejea kweli, kiwango kimeonekana kuwa cha hali ya ju