MFUMO WA 3-5-2 NDIYO SILAHA YENYE SUMU KALI KWA SIMBA



Ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Singida United umempa nafasi ya kuzungumza Kocha Msaidizi wa Simba, Mrundi Masoud Juma ambaye amesema kuwa wachezaji wameanza kuuzoea mfumo wake mpya na kuwazodoa waliokuwa wakimpinga awali.
Akiiongoza Simba katika michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya Joseph Omog kuondolewa, Djuma alishindwa kuifanya Simba kutamba na matokeo yake ikaonekana kuwa ni timu ya kawaida.
Kutofanya vizuri katika michuano ya Kombe la Mapinduzi kukasababisha baadhi ya mashabiki na wadau wa timu hiyo kuona kocha huyo hafai, lakini kiwango kizuri dhidi ya Singida United, Alhamisi iliyopita kimerejesha imani ya Wanasimba wengi kwa kocha huyo msaidizi.
Mara baada ya mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar ea Salaam, Djuma alisema mfumo wa 3-5-2 unahitaji wachezaji kujituma zaidi na wanapofika kwenye eneo la 18 la wapinzani wanatakiwa kushambulia sana, lakini wachezaji walikuwa hawajazoea kwa kuwa lilikuwa suala jipya kwao. 
Amesema mchezo huo haikuwa rahisi kwao lakini matokeo hayo ni kutokana na kutokata tamaa kwani watu waliongea sana juu ya mfumo mpya ndiyo maana timu ilifanya vibaya Mapinduzi lakini ilitakiwa uvumilivu.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!