JUMA NYOSSO NA JOHN BOCCO WAMEKUTANA LIVE LEO UWANJA WA KAITABA
Simba wanatarajiwa kuwa wageni wa Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom, leo Jumatatu kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.
Katika mchezo huo SImba itakuwa ikiwania kurejea kileleni katika msimamo wakati Kagera Sugar ikipambana kukwepa kushuka daraja.
Kocha Mecky Maxime ambaye ni bosi wa Kaggera Sugar amefunguka kuwa timu yake ipo swa kwa ajili ya mchezo huo akiwemo beki wake wa kati, Juma Nyosso.
Ikumbukwe kuwa Juma Nyosso aliwahi kufungiwa kutocheza soka kwa miaka miwili kutokana na kumfanyia kitendo cha kidhalilishaji mshambuliaji John Bocco aliyekuwa Azam FC kipindi hicho.
Nyosso atakuwa na kazi ngumu ya kuwadhibiti washambuliaji wa Simba akiwemo Bocco ambaye kwa sasa yupo Msimbazi wengine ni Emmanuel Okwi raia wa Uganda.
Maxime amesema kikosi chake kipo fiti na wanachohitaji ni pointi tatu tu katika mchezo huo, huku akijinadi kuwa hawana hofu ya kuikabili Simba ambayo ndiyo kinara wa ligi kuu.
Comments
Post a Comment