KOCHA WA URA ASEMA BORA AKUTANE NA SINGIDA UNITED KULIKO YANGA NUSU FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI
Kocha wa URA Nkata Paul amesema kama timu yake itafanikiwa kusonga mbele kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi asingependa kukutana na
Yanga.
Yanga.
URA na Simba zilitarajiwa kupambana jana jioni na mshindi katika mchezo huo ataungana na Azam FC, kucheza nusu fainali ya michuano hiyo
ambayo itapigwa Januari 10 Uwanja wa Amaan hapa Zanzibar.
ambayo itapigwa Januari 10 Uwanja wa Amaan hapa Zanzibar.
Nkata, ameiambia Goal, Yanga ndiyo timu ambayo anaihofia kukutana nayo kutokana na mfumo wanaotumia na wachezaji
waliokuwa nao ambao siyo rahisi kuwadhibiti kutokana na kubadilika mara kwa mara.
waliokuwa nao ambao siyo rahisi kuwadhibiti kutokana na kubadilika mara kwa mara.
"Kitu kinachonifanya kuihofia Yanga kwanza ni timu ambayo huwezi kuikariri kila siku inakuja na kikosi kipya na wachezaji wake wengi ni
vijana wana kasi na nguvu za kupambana ukilinganisha na timu nyingine hicho ndiyo kina nifanya niwe na hofu ya kukutana nao," amesema Nkata.
vijana wana kasi na nguvu za kupambana ukilinganisha na timu nyingine hicho ndiyo kina nifanya niwe na hofu ya kukutana nao," amesema Nkata.
Kocha huyo amesema anatambua kwamba Yanga inawakosa baadhi ya wachezaji wake wenye uzoefu na majina makubwa lakini vijana waliopo
kwake yeye ndiyo anaona ni hatari kuliko wachezaji hao ambao wangeifanya timu kutokuwa na tofauti na klabu za Simba na Azam.
kwake yeye ndiyo anaona ni hatari kuliko wachezaji hao ambao wangeifanya timu kutokuwa na tofauti na klabu za Simba na Azam.
Pamoja na yote kocha huyo alisema kama itatoke wakakutana na Yanga basi atalazimika kubadili mfumo wa uchezaji kwa timu yake na kutumia
sana uzoefu wao ili kuweza kushinda mchezo huo na kutinga fainali kwa mara nyingine kama walivyofanya mwaka juzi ambapo waliifunga Yanga kwa
mikwaju ya penalti na kucheza fainali na Mtibwa Sugar.
sana uzoefu wao ili kuweza kushinda mchezo huo na kutinga fainali kwa mara nyingine kama walivyofanya mwaka juzi ambapo waliifunga Yanga kwa
mikwaju ya penalti na kucheza fainali na Mtibwa Sugar.
Tayari URA imeifunga Azam kwenye mchezo wa hatua ya makundi na kocha huyo tayari alishatamba kuifunga Simba katika mchezo wao wa jana jioni
ili kudhihirisha kwamba timu hizo ninyepesi kwake ingawa watu wanaziona bora kuliko Yanga.
ili kudhihirisha kwamba timu hizo ninyepesi kwake ingawa watu wanaziona bora kuliko Yanga.
Comments
Post a Comment