MANARA ALICHOKISEMA BAADA YA USHINDI WA SIMBA SC JANA


Simba ilipata ushindi wa mabao  4-0 dhidi ya Majimaji, jana Jumapili katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, baada ya ushindi huo kama kawaida Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alikuwa na jambo la kusema.
Ikumbukwe kuwa katika ushindi huo mabao ya Simba yalifungwa na John Bocco na Emmanuel Okwi, kila mmoja alifunga mawili.
Bocco ndiye ambaye alionyesha kiwango kizuri zaidi kwa kuwa pia alitengeneza bao moja la Okwi.
Sasa kama kawaida yake Manara akayasema haya: 
“Idadi ya magoli ya wahenga John Bocco na Emmanuel Okwi ni sawa na idadi ya magoli yote waliyofunga Gongowazi hadi sasa..nadhani sasa mtaelewa maana ya kikosi cha one B, goli 35.points 35 kisha unbeaten. Nisisahau, endeleeni pia kujiongopea eti mtatukuta, hivi Kwani zile mbeleko za jamaa yenu zipo safari hii?Shubamit!!!! “
Aidha, manara pia alitoa kauli hii:
“Niseme nn zaidi ya kumshukuru Mungu..Alhamdulillah.....uzuri wake tunashinda kisha tunawapa burudani washabiki..wale walionuna Fansida 20 ukichanganya na balimi mixer viroba vnne ni tiba sahihi.”

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!