DIRISHA DOGO LIMEFUNGULIWA LEO, HAWA NDIYO WANAOWANIWA KWA UKARIBU
Usajili wa dirisha dogo unatarajia kufunguliwa leo na kumekuwa na presha kubwa kuhusu wachezaji wanaotakiwa kutoka upande mmoja kwenda mwingine.
Hawa ni baadhi ya wachezaji wanaowaniwa na klabu mbalimbali katika dirisha hili la usajili.
Mohamed Rashid: Nyota wa Tanzania Prisons amegeuka lulu kwenye Ligi Kuu baada ya mechi 9 za awali hadi sas, uwezo wake mkubwa wa kufumania nyavu umewashangaza wengi , magoli 6 katika mechi 9.
Mohamed Issa: Tayari klabu za Simba na Yanga zimeonesha nia ya kumtaka kiungo huyo mchezeshaji wa Mtibwa Sugar mwenye uwezo mkubwa wa kumiliki mpira na kupiga pasi sahihi bila kupoteza
Ramadhani Kihimbwa: Winga wa Mtibwa Sugar ametokea kuvivutia baadhi ya klabu kubwa hapa nchini baada ya kuonesha uwezo mkubwa katika robo ya kwanza ya Ligi kuu
Eliud Ambokile: Straika wa Mbeya City anatazamiwa kuwa lulu kwenye dirisha dogo kufuatia kasi yake aliyoionesha ya kufumania nyavu, tayari amefunga mabao 4 katika mechi 9.
Comments
Post a Comment