Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!



 ACHANA na mechi ya Man city na Spurs, ngoma leo saa 1 usiku iko kwenye Uwanja wa Taifa kwa Simba na azam. Kwa lugha rahisi ni kwamba wenye mpira wao Tanzania wanafungua msimu mpya kwa burudani ya Ngao ya Jamii.

Kuanzia nje mpaka ndani ya Uwanja hizi ndizo klabu zenye bajeti kubwa zaidi na leo zinakutana Taifa kuonyeshana ubabe na kufungua njia mpya. Ni mechi ngumu na itakayokuwa na utamu wa aina yake. Ni lazima mtu akae, hakuna cha sare wala suluhu.

Mtaalam Razack Abalora atasimama kwenye lango la Azam huku pembeni katika ulinzi wakisimama Nicholas Wadada na Bruce Kangwa.

Pale kati atakuwepo Daniel Amoah na Oscar Masai. Kati yupo Yakub Mohammed, Abdallah Masoud, Salmin Hoza, Salum Aboubakary ‘Sure Boy’ na Idd Seleman. Huyu ni wakuitwa Nado. Pale mbele anamalizia Obrey Chirwa mwenyewe. Simba sasa. Aishi Manula hayuko fiti.

Beno Kakolanya ataanza chini ya ulinzi wa Shomari Kapombe,Hussein Mohammed ‘Tshabalala’, Pascal Wawa na Tairone Dos Santos. Kuna mtu anaitwa Al Sharaf Shiboub, Chama na Dilunga hawa watauchezea sana hapo kati leo.

Mastraika sasa Meddie Kagere, John Bocco na Deo Kanda. Sasa kwa huo muziki, mechi ya Man City na Spurs ya nini? Twendeni Taifa. Mechi hiyo itahusisha makocha na wachezaji kutoka mataifa 12 ambayo ni Ivory Coast, Burundi, Ghana, Rwanda, Sudan, Brazil, Zambia, Zimbabwe, DR Congo, Kenya, Ubelgiji na Tanzania. Pambano hilo ni sehemu ya ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu Bara unaoanza
Agosti 24, mwaka huu ambayo itashirikisha timu 20.

Kocha Mkuu wa Simba Mbelgiji, Patrick Aussems alisema mechi hiyo haitakuwa nyepesi kwao kutokana na ubora wa wapinzani wao, lakini anaamini timu yake itapambana na kupata matokeo mazuri.

Aussems alisema kuwa, anapata matumaini ya kupata matokeo mazuri baada ya wachezaji wake waliokuwa majeruhi ambao ni kipa Aishi Manula, Wilker Dos Santos na Ibrahim Ajibu kupona na kuanza mazoezi na timu.

“Tayari nimekifanyia marekebisho kikosi changu kwenye baadhi ya sehemu ili kuhakikisha tunapata matokeo mazuri na kikubwa niwaombe mashabiki wa Simba wajitokeze kwa wingi kama ilivyokuwa Simba Day tulivyocheza na Power Dynamo.

“Hadi hivi kikosini kwangu sina majeruhi yeyote baada ya Ajibu, Manula na Wilker kupona majeraha yao yaliyokuwa yanawasumbua na kusababisha kuukosa mchezo uliopita wa Ligi ya Mabingwa Afrika na Ud Songo ya Msumbiji,” alisema Aussems.

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Azam FC, Etiene Ndayiragije alisema kuwa, wamepanga kuutumia mchezo wao huo kama sehemu ya maandalizi ya mechi yao ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Fasil Kenema ya Ethiopia itakayopigwa Agosti 24, jijini Dar.

“Ili tuvuke hatua hii ya raundi ya awali ya Kombe la Shirikisho ni lazima tuwafunge Simba na hilo linawezekana kutokana na ubora wa kikosi changu.

“Nitawakosa wachezaji wawili pekee ambao ni Aggrey Morris na Mudathiri Yahaya wenye majeraha, lakini wengine wote wapo vizuri kwa ajili ya pambano hilo,” alisema Ndayiragije ambaye anasifika kwa uwezo wa kuusoma mchezo na kubadili matokeo.

Comments

  1. Casino - No Deposit Bonus - Casinoowed
    No Deposit Bonuses septcasino and Promotions · 100% Match bonus up to €200 · Free 인카지노 spins, no deposit bonus code, 10x playthrough, no deposit bonus · หาเงินออนไลน์ 100%

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

MATOLA: TULIENI NIWAONYESHE NAMNA SIMBA INAVYOFUNGWA

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji