MANENO YA KOCHA MSAIDIZI WA KIKOSI CHA STAND UNITED KUHUSU KIFO CHA NTAMBI.
Kocha msaidizi Wa kikosi cha Stand United ya mkoani Shinyanga Athumania Bilali (Bilo) amepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha aliyekua kocha msaidizi Wa kikosi cha Mwadui fc Jumanne Ntambi aliyefariki usiku wa tarehe 24 Januari mkoani Shinyanga.
Akizungumza na Shutikali Kocha Bilali amesema ameumia sana na kifo cha Kocha Ntambi kwani amewahi kumfundisha katika timu ya Biashara Shinyanga Mnamo Mwaka 1992
"Hakika kifo cha Jumanne Ntambi kimesikitisha sana kwani alikua mwalimu Wangu katika timu ya Biashara Shinyanga pia ndiye aliyenishawishi Mimi kuingia katika kazi Hii ya ukocha"
Akimuelezea kocha Ntambi Bilali amesema alikua ni Kocha Mwenye kujali kazi Yake na alikua ni Kocha aliyekua akiheshimu kila mtu hata kama amemzidi Mafanikio huku akiwataja nyota kadhaa waliopita kwenye mikono yake akiwemo Mshambuliaji wa zamani wa Kahama United Karume Songoro.
Jumanne Ntambi alifariki Siku ya jumatano ya 25 saa Tatu za usiku akiwa mkoani Shinyanga na Mwili wake kusafirishwa mpaka mkoani Moshi alikohifadhiwa katika makaburi nyumbani kwao amewahi kuwa katika Darasa moja la ukocha na Johnson Tegete pamoja na Silivester Marsh ambaye hivi sasa ni marehemu,huku akizifundisha timu za Biashara Shinyanga,timu ya mkoa Wa Shinyanga Maarufu kama Igembe Nsabo pamoja na timu ya Mwadui fc.
Mungu ailaze roho ya Marehemu Jumanne Ntambi Aaaamin!
Comments
Post a Comment