KAGERA SUGAR IMETOA MAAMUZI BAADA YA JUMA NYOSO KUMPIGA SHABIKI


Wakati sakata la beki wa Kagera Sugar, Juma Nyoso kushikiliwa na Jeshi la Polisi la mkoani Kagera kutokana na kudaiwa kumshambulia shabiki na kusababisha apotezea fahamu kwa muda, kuna tamko limeolewa kutoka kwenye klabu yake.
Ikumbukwe kuwa Nyoso anatuhumiwa kumshambulia shabiki huyo ambaye jina lake linatambulika kwa jina la Shabani Hussein tukio lililotokea muda mfupi baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Kagera Sugar dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.
Taarifa kutoka ndani ya Kagera Sugar zinaeleza kuwa uongozi wa klabu hiyo umeamua kutomchukulia hatua yoyote Nyoso ambaye aliachiwa Jumanne ya wiki hii kwa dhamana kutoka katika mikono ya jeshi la polisi.
Kigogo mmoja wa Kagera Sugar amenukuliwa akisema kuwa suala hilo kwao litamalizwa ndani ya klabu kwa kuwa hawataki liwe la watu wote na hawana mpango wa kumchukulia hatua zozote za kinidhamu.
Kwa kauli hiyo sasa Nyoso anasubiri mwendelezo wa pande mbili ambazo ni polisi kwa kuwa ni tukio lililohusisha kumpiga raia mara baada ya mchezo lakini pia anaweza kuadhibiwa na Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) kwa kuwa alimshambulia shabiki ndani ya eneo la uwanja huo wa Kaitaba.
Katika mchezo huo ambapo tukio lilitokea, Simba ilipata ushindi wa mabao 2-0 wafungaji wakiwa ni Said Ndemla na John Bocco.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!