AZAM FC YATINGA FAINALI MAPINDUZI CUP, YAITUNGUA SINGIDA UNITED 1-0


Mshambuliaji Shaaban Idd amekuwa shujaa kwa upande wa Azam FC usiku huu baada ya kufunga bao pekee dhidi ya Singida United katika ushindi wa 1-0 lililoipeleka timu yake kwenye fainali ya Kombe la Mapinduzi.
Hiyo ni fainali ya pili mfululizo kwa mabingwa hao watetezi wa michuano hiyo baada ya mwaka jana kutinga fainali na kuichapa Simba bao 1-0, lililofungwa na nahodha Himid Mao ‘Ninja’.
Kwa matokeo hayo, Azam FC itakutana na URA ya Uganda kwenye mechi ya fainali itakayofanyika Jumamosi ya Januari 13, mwaka huu kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Mechi hiyo itakumbushia mchezo wa Kundi A ambao ulihusisha timu hizo na Azam FC kupoteza kwa bao 1-0, lililofungwa na Nicholas Kagaba, hiyo inamaanisha kuwa timu bora za michuano hiyo zilizoingia fainali zimetoka kundi hilo.
Mabadiliko yaliyoibeba Azam FC hadi kushinda mchezo huo wa nusu fainali uliochezwa jana usiku yalikuwa ni ya kuwaingiza viungo Frank Domayo, winga Idd Kipagwile, na yale ya dakika za mwisho yaliyozaa bao ya Shaaban na kiungo mkabaji Braison Raphael.
Bao hilo lilifungwa dakika ya 78 na Shaaban aliyetumia vema mpira wa kurushwa wa Bruce Kangwa, kabla ya kuupokea na kuwazidi maarifa mabeki wa Singida United na kupiga shuti safi la juu lililomshinda kipa Peter Manyika.
Azam FC inaingia fainali baada ya kucheza mechi tano, nne za makundi ikishinda tatu dhidi ya Mwenge (2-0), Jamhuri (4-0) na Simba (1-0) ikipoteza mmoja dhidi ya URA (1-0) kabla ya nusu fainali kuichapa Singida United.
Kikosi cha Azam FC:
Razak Abalora, Himid Mao (C), Bruce Kangwa, Agrey Moris, Yakubu Mohammed, Stephan Kingue/Frank Domayo dk 46 , Joseph Mahundi/Braison Raphael dk 76, Salmin Hoza, Yahya Zayd/Shaaban Idd dk 76, Bernard Arthur, Enock Atta/Idd Kipagwile dk 46

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!