KAULI KUTOKA KWA MASOUD DJUMA KUHUSU KOCHA MFARANSA WA SIMBA
Klabu ya Simba imemshusha nchini Kocha Pierre Lechantre raia wa Ufaransa kwa ajili ya kuinoa timu hiyo lakini kuna kauli kutoka kwa Masoud Djuma ambaye ndiye aliyekuwa akikaimu nafasi ya kocha mkuu klabuni hapo.
Djuma alikuwa akiiongoza Simba kwa muda baada ya klabu hiyo kumtimua kazi Kocha Joseph Omog ambapo sasa imeshusha kocha mkongwe mwingine Pierre Lechantre ambaye ni raia wa Ufaransa.
Kocha huyo Mfaransa ambaye ametua jijini Dar es Salaam akiwa na kocha wa mazoezi ya viungo, Mohammed Aymen Hbibi raia wa Morocco, kwa pamoja wamekaribishwa na ushindi wa mabao 4-0 wakati Simba ilipocheza dhidi ya Singida United.
Akizungumzia ujio huo, Djuma ambaye ni raia wa Burundi alisema kwanza anamkaribisha sana na anampa maelezo yote juu ya timu tangu alipoikuta na mabadiliko aliyofanya.
Alisema baada ya hapo iwapo ataamua kuendelea na mfumo wa sasa alioanzisha yeye ni sawa na kama ataamua kubadilisha na kuja na falsafa yake yote kwake ni sawa.
"Mimi sina tatizo kabisa, namkaribisha sana, nitampa maelezo yote ya timu tangu nimekabidhiwa na iwapo akiona inafaa kuendelea na mfumo wa sasa au kubadili na kuleta wake yote kwangu ni sawa," alisema Djuma.
Comments
Post a Comment