DALALI: KUNA TATIZO SIMBA, TUKIENDELEA HIVYO TUTAKOSA UBINGWA


Kutokana na mwenendo wa timu ya Simba kuonekana ni wa kusuasua, Mwenyeketi wa zamani wa Klabu ya Simba, Hassan Dalali amekuja juu na kutupa lawama kwa viongozi na wachezaji wa timu hiyo.
Dalali amesema kuwa anashangazwa na mwenendo mbaya wa timu yake huku akiwataka viongozi kuzungumza na wachezaji wao kujua kuna tatizo gani, siyo kukaa kimya huku mambo yakiendelea kuharibika.
“Kuna mgogoro wa ndani kwa ndani, kama kweli upo basi ni vema uongozi wakaufanyia kazi mapema na siyo kusubiri hadi mambo yawe makubwa.
“Wao viognozi wanatakiwa kukutana na kumalizana kiutu uzima, pia wanaweza kukaa pamoja na wachezaji wao kujua tatizo ni nini.
“Kitu kingine wachezaji wanatakiwa kujiuliza, kwani Simba ni klabu kubwa, Wanasimba wote tunataka ubingwa, sasa mambo wanayoyafanya hayaendani na ukubwa wa klabu hii.
“Wachezaji wanatakiwa kusema kama kuna tatizo au la, haya mambo yakiendelea kimyakimya yatasababisha tukose ubingwa,” alisema Dalali.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!