ELIAS MAGURI BADO AMEKWAMA KUJIUNGA NA POLOKWANE CITY YA AFRIKA KUSINI
Mshambuliaji wa Mtanzania Elias Maguri ameendelea kuonekana katika mitaa ya Dar es Salaam baada ya dili lake kukwama kujiunga katika timu ya Polokwane City inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini.
Awali ilielezwa kuwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba na Stand United aliyekuwa akicheza soka Uarabuni, alikuwa mbioni kujiunga na Yanga lakini mambo yakabadilika na akaelekea Afrika Kusini ikielezwa anaenda kujiunga katika timu ya Polokwane City.
Maguri amesema ni kweli alishamalizana na Polokwane City kwa kuwa alishasaini mkataba wa awali kabla ya kwenda kushiriki katika michuano ya Kombe la Chalenji nchini Kenya lakini baadaye hawakukubaliana katika masuala ya maslahi.
Amesema kuwa makato ambayo klabu hiyo iliyaibua katika dakika za mwisho ndiyo yalisababisha yeye kutosaini mkataba wa kuichezea timu hiyo.
Kuhusu mipango yake, amesema anaendelea kusikilizia ofa kabla ya kuchukua maamuzi ya wapi pa kwenda.
Comments
Post a Comment