HAYA NDO MANENO YA MAJIMAJI KUHUSU MECHI YAO NA SIMBA



Kuelekea mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba dhidi ya Majimaji, Jumapili hii kuna tambo zimetolewa na straika wa Majimaji, Jerry Tegete.
Jerry Tegete ambaye ni nyota wa zamani wa Yanga amedai kuwa timu yao ipo fiti kuelekea mchezo huo na kuwakumbusha Simba kuwa wenzao, Yanga waliponea chupuchupu wakati walipokutana na Majimaji katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma.
Ikumbukwe kuwa Majimaji na Yanga zilitoka sare ya bao 1-1 ambapo Yanga ililazimika kutoka nyuma kupata sare hiyo.
Simba kwa sasa ipo chini ya Kocha Mkuu mpya Pierre Lechantre raia wa Ufaransa ambaye anatarajiwa kukaa kwa mara kwanza kwenye benchi la timu hiyo katika mchezo huo wa Jumapili.
Akizungumzia mchezo huo utakaichezwa kwenye Uwanja wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Tegete alisema kuwa ujio wa kocha huyo mpya hauwafanyi wao waogope na kupata matokeo mabaya, kwani wataingia uwanjani kwa ajili ya ushindi pekee.
Tegete alisema, katika kuhakikisha timu yao inamaliza ligi katika nafasi nzuri ni lazima washinde kila mechi watakayokutana mbele yao kwa lengo la kufikia malengo yao.
Tegete ambaye ni mwenyeji wa Mwanza amesema ligi inaelekea katika mzunguko wa pili, hivyo ni lazima wao washinde michezo yote iliyopo mbele yao ili tujiweke katika nafasi nzuri ya msimamo.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!