RAIS SIMBA ATOA TAMKO KUHUSU KOCHA, KICHUYA & MKUDE


Baada ya kikosi cha Simba kufanya vibaya na kutolewa mapema kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi uongozi wa klabu hiyo umesema hauna mpango wa kumtimua kocha wao Masoud Djuma, kwa sababu hawaamini kama yeye ndiye aliyechangia timu yao kufanya vibaya.
Kaimu Rais wa Klabu ya Simba, Salim Abdallah amefunguka kuwa bado wanaimani na kocha huyo pamoja na mifumo yake ya ufundishaji isipokuwa watahakikisha wanamletea kocha mkuu ili aweze kusaidiana naye ili timu iweze kurudi kwenye mwenendo wake uliozoeleka.
Kaimu rais huyo amesema Masoud ni kocha mzuri na bado wana imani naye ila wapo kwenye mchakato wa kutafuta kocha mkuu ambaye watasaidiana kwa ajili ya kuleta mafanikio klabuni hapo.
Kiongozi huyo amesema pia kitu kingine ambacho wamekusudia kukifanya ni kuwaita na kuwahoji wachezaji ambao walionyesha utovu wa nidhamu kwenye michuano hiyo katika mchezo wa mwisho dhidi ya URA, na ikigundulika walifanya makosa watawaadhibu kwa mujibu wa sheria na kanuni za klabu yao.
Wachezaji wanne walisusa kukaa benchi katika mchezo dhidi ya URA, baada ya kufanyiwa mabadiliko na nafasi zao kuingia wengine wachezaji hao ni Shiza Kichuya, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto na Nicholaus Gyan.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!