AZAM FC 1-2 YANGA SC

Image result for azam 1-2 yanga

Azam Wanatoka uwanjani vichwa chini
MPIRA UMEKWISHA
Dk 92, Chirwa anapiga krosi pale lakini inaokolewa
 Dk 92, Juma Mahadhi anawekwa chini na inakua ni faulo
DAKIKA ZA NYONGEZA
Dk 90+3, Yanga wanapoteza nafasi pale baada ya Mwashiuya kupiga shuti lilitoka nje ya goli
Dk 88, Kelvin Yondani yuko chini baada ya kuruka na kutua vibaya na mguu wake, anapewa huduma ya kwanza 
DK 87, Salmin Hoza anapiga mpira na unakwenda nje bila madhara yoyote 
Dk 85, Hassan Kessy anafanyiwa madhambi na unapigwa kuelekea Azam
Dk 85, Mahundi anapiga faulo lakini inaokolewa na Yanga
Dk 84, Himid Mao anawekwa chini na inakua faulo 

Dk 81, KADI NYEKUNDU   Salum Abubakar Salum anapewa kadi nyekundu kwa kumsukuma Hassan Kessy baada ya kuwa na kadi mbili za njano
Dk 77, KADI YA NJANO nyingine inakwenda kwa Aggrey Moriss baada ya kucheza rafu
Dk 76, KADI YA NJANO  kwa  Kelvin Yondan anapewa na ni kadi ya  pili kwa Yanga baada ya kumchezea rafu Mbaraka Yusuph
Dk 75, Geofrey Mwashiuya anaambiwa amejenga kibanda na inakua offside
Dk 74, KADI YA NJANO Kuna zogo limetokea hapa, na Papi Kabamba Tshishimbi anapewa kadi ya njano
Dk 73, Azam wanatawala hivi sasa katika eneo la kati la uwanja
Dk 71, Shuti la Mbaraka Yusuph linakua nyanya kwa Rostand 
Dk 68, MABADILIKO   Juma Mahadhi anakwenda kuchukua nafasi ya Ibrahim Ajibu anayekwenda benchi
Dk 67, Faulo ya Atta Agyei inaokolewa na golikipa Rostand
Dk 66, MABADILIKO Geofrey Mwashiuya anaingia kuchukua nafasi ya Emmanuel Martin 
 Dk 65, MABADILIKO Paul Peter anaingia kuchukua nafasi ya Shaban Chilunda, mfungaji wa goli la Azam
 Dk 62,  Ndani ya 18 pale Azam wanapiga mpira lakini unaokolewa na mabeki, mawasiliano hafifu ya Chilunda na Mbaraka Yusuph yanawakosesha nafasi
Dk 60, Martin anawatoka mabeki wawili wa Azam, anagongeana na Ajibu vizuri lakini kipa Abarola anakuwa mjanja
Dk 58, Ajibu anafanyiwa madhambi na inakwenda kupigwa faulo 
Dk. 57, Yakubu Mohamed aliingiza krosi lakini shuti la Atta Agyei linakua fyongo
DK 55. Mabadiliko yanafanyika kwa Azam, anatoka Stephen Kingwe anaingia Mbaraka Yusuph
Dk 49. Kangwa anamtoka tena Kessy na kumimina krosi safi kabisa, goal kick
Dk 46. Chirwa anawekwa chini na Nkongo anasema ni madhambi. Anaupiga vizuri Gadieal na Yanga wanaonekana kama wameanza kwa kasi nzuri
 Dk 45. Yanga ndiyo wanaanza na kujaribu shuti lakini ni dhaifu

MAPUMZIKO
DAKIKA 2 ZA NYONGEZAGOOOOOOOOOO Dk 44, shuti kali la Gadiel Michael linakwenda moja kwa moja wavuni baada ya kumshinda kipa wa Azam FC
KADI Dk 43 Kingu naye analambwa kadi kwa kumuangusha Makapu
Dk 42, shambulizi jingine zuri la Yanga lakini Razak anadaka vizuri mkwaju wa faulo wa Martin
Dk 39 Kangwa anamgongea mpira Kessy na kuwa kona, inachongwa tena na Kangwa inakuwa haina faida
SUB Dk 36, Azam FC wanamuingiza Salim Hoza kuchukua nafasi ya Benard Arthur
Dk 35, Martin anajaribu vizuri hapa, mpira wake unatoka juu kidogo ya lango la Azam  FC
Dk 33 mpira umesimama, Tshishimbi anatibiwa baada ya kugongana na Kingu
GOOOOOOOO Dk 30, Ajibu anatoa pasi nzuri kabisa kwa Chirwa anayeuwahi mpira mbele ya kipa wa Azam na kuukwamisha wavuni kwenye nyavu zilizo wazi
Dk 28, Ajibu akiwa mbali anajaribu vizuri kabisa, lakini kipa Abarola yuko makini kabisa
Dk 26, Azam FC inabidi wajihadhari kutokana na kucheza faulo nyingi mfululizo
Dk 24 Kessy anakwatuliwa na Kangwa mbele ya mwamuzi wa akiba, lakini anaonekana kama hakuona. Yuko nje anatibiwa
KADI Dk 22, Sure Boy analambwa kadi kwa kumuangusha Martin


Dk 20, Yanga bado wako katika lango la Azam, wanagongeana vizuri lakini Ajibu anapiga juu na kuwa goal kick
Dk 19, Yanga wanafanya shambulizi jingine zuri, Tshishimbi anagongeana na Ajibu na Chirwa anaachia mkwaju unatoka pembeni kidogo
Dk 17, Kangwa tena, anaingiza krosi nyingi nzuri, Yondani anaruka na kupiga kichwa anaondosha
Dk 16 Kangwa anamzidi tena ujanja Kessy, anaingiza krosi safi hapa, Yanga wanaokoa
Dk 15, Yanga wanagongeana vizuri kabisa, Tshishimbi anaachia mkwaju matata kipa Azam anadaka na kutema, lakini anauwahi tena


Dk 12, shambulizi jingine pole la Azam FC, Arthur anaachia mkwaju hapa lakini ni chakula kwa Rostand
KADI Dk 10, Chilunda anamkwatua Kessy na mwamuzi Nkongo anamramba kadi ya njano ya kwanza katika mechi ya leo Dk 7, Yanga tena, pasi nzuri ndani ya 18, lakini Tshishimbi anachelewa
Dk 5, Ajibu anajaribu mkwaju hapa lakini unakuwa dhaifu kabisa
GOOOOOOOOOO Dk 3, Kangwa anamtoka Kessy, anamtoka Raphael Daud na kuingiza krosi safi kabisa, Iddi anaunganisha na kuandika bao la kwanzaDk 2, Kessy anachuana vizuri na Kangwa na kumzidi maarifa, inakuwa goalkick




Dk 1, Yanga wanaanza na kufika katika lango la Azam FC, wanaokoa, nao wanaanza kushambulia kwa kasi

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!