MANENO YA KOCHA WA MAJIMAJI KUHUSU MECHI YA SIMBA NA MAJIMAJI ITAKAYOPIGWA WIKENDI HII KWENYE UWANJA WA TAIFA

Image result for majimaji fc

Kikosi cha Majimaji kinatarajiwa kjuwasili jijini Dar es Salaam, leo Alhamisi kwa ajili ya kuvaana na wapinzani wao, Simba katika pambano la Ligi Kuu ya Vodacom ambalo litapigwa wikiendi hii kwenye Uwanja wa Taifa.
Ofisa Habari wa Majimaji, Onesmo Ndunguru ambaye timu yake inadhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya Sokabet amesema mipango yao ni kuwasili Dar Alhamisi hii wakiwa na kikosi kamili kwa ajili ya mchezo huo na Simba.
Onesmo amesema wanatua Dar ili kupata pointi tatu kwa kuwa wanajua mchezo huo ni muhimu kwao.
Alipoulizwa juu ya maandalizi yao kuelekea mchezo huo, Kocha wa Majimaji, Habib Kondo alisema: “Tunajua kwamba mchezo utakuwa mgumu ila tumejipanga vyema kwa ajili ya kupata pointi mbele ya wenzetu hao, tunakuja tukiwa kamili kwa maana ya kikosi chote na siku chache ambazo tutakaa huko zitatufanya kuzoea mazin­gira kabla ya kupambana na wapinzani wetu.”

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!