YANGA YAIFANYIA UMAFIA URA

Image result for yanga sc 2017

YANGA SC leo inashuka dimbani kucheza mechi ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya URA ya Uganda, lakini siku moja kabla ya mechi, Wanajangwani hao wameamua kufanya umafia mkubwa ili waweze kupata ushindi.
Yanga inatarajiwa kushuka dimbani leo kwenye Uwanja wa Amaan saa 10:30 jioni, katika mechi ya nusu fainali ya kwanza kwenye mashindano hayo dhidi ya Waganda hao.
Iko hivi; uongozi wa Yanga baada ya kuona timu imetinga hatua ya nusu fainali, umeamua kukiongezea nguvu kikosi chake kilichoko Zanzibar kwa kutuma majeshi zaidi yatakayowachunguza URA na kusaidia kuongeza mbinu za ushindi kwa timu hiyo ya Jangwani.
Yanga ambayo haijafungwa mechi hata moja kwenye michuano hiyo, inataka kuendeleza wimbi la ushindi ili kutimiza dhamira yao ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi unaotetewa na Azam FC.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!