YANGA YAITAMANI AZAM NUSU FAINALI YA KOMBE LA MAPINDUZI

Kocha msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amesema hawana timu ambayo inawatisha kwenye michuano hiyo na wapo tayari kucheza na timu yoyote
Baada ya kufanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapindu, kocha msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa, amesema kamwe
hawaihofii timu yoyote katika michuano hiyo.
Nsajigwa ameiambia Goal,  kuwa wanashiriki  michuano hiyo wakiitumia kama mazoezi na kujiweka fiti kwa ajili ya michuano inayowakabili mbeleni na kamwe hawapo kwa ajili ya kuihofia timu nyingine na watakao kuja mbele yao wao watambana kadri ya uwezo wao bila kujali matokeo baada ya dakika 90.
"Tumekuja kushiriki michuano hii lengo letu ni kufanya vizuri tunashukuru leo tunapata ushindi wa nne mfululizo niwapongeze
wachezaji wangu kwa kujituma na kupata matokeo haya naamini hata kwenye mechi zijazo tutafanya vizuri hatuna hofu na timu yoyote hata
kama hatuna wachezaji wenye majina makubwa kwenye kikosi chetu," amesema Nsajigwa.
Kocha huyo ambaye anamsaidia George Lwandamina aliyepo kwao Zambia alikokwenda baada ya kufiwa na mwanae, amesema wanachotaka kuona ni
uwajibikaji wa wachezaji wao na kupata uzoefu wa kutosha kutokana na malengo waliyokuwa nayo kwenye michuano ya kimataifa.
Katika michuano ya Kombe la mwaka huu asilimia kubwa ya kikosi cha Yanga ni wachezaji chipukizi waliochangaywa na wazoefu huku wale wakongwe kama Thabani Kamusoko, Donald Ngoma Amissi Tambwe, Kelvin Yondani na Obrey Chirwa wakionekana kukaa benchi bila kutumika.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!