IMANI ZA KISHIRIKISHA ZAMTESA STAA WA KIMATAIFA WA SIMBA
Wakati mshambuliaji Nicholas Gyan raia wa Ghana aliposajiliwa na Simba, mwaka jana, ilielezwa kuwa ani mmoja wa wachezaji chipukizi wenye vipaji vya juu katika soka.
Pamoja na sifa hizo bado Gyan alishindwa kuwika katika timu hiyo huku wadau wengi wa Simba wakikosa majibu sahihi ya kutoa juu ya mchezaji huyo.
Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Masoud Djuma amesema, wakati anaingia Simba alikuwa haamini kama Nicholas Gyan ni mchezaji mzuri lakini baada ya kukaa na kuzungumza na mchezaji huyo alimwambia kwamba ameambiwa anarogwa ndiyo maana anashindwa kufanya vizuri.
Kocha huyo aliyasema hayo mara baada ya Gyan kuonyesha kiwango cha juu katika mchezo dhidi ya Singida United ambapo Simba ilipata ushindi wa mabao 4-0.
Anasema wakiwa mazoezini alipata nafasi ya kuzungumza na kumshauri mchezaji huyo kuachana na imani hizo za kurogwa, na kweli hilo likatimia, akaonyesha uwezo mzuri mazoezini, baadaye akapata nafasi ya kuonyesha uwezo wa juu katika mchezo dhidi ya Singida United.
Djuma pia amesisitiza kuwa hampangi mchezaji kwa sababu ya jina au undugu ndiyo maana Laudit Mavugo licha ya kuwa ni Mrundi mwenzake lakini hachezi kwa sababu hayuko fiti, atakapokuwa sawa atapata nafasi ya kucheza.
Comments
Post a Comment