ALIYEWAUA YANGA, AMTISHIA AMANI EMMANUEL OKWI



BAADA ya kufanya vizuri katika mwezi Desemba kwa kufunga magoli saba katika michezo miwili aliyoichezea timu Mbao FC, hatimaye kufanikiwa kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom,
mshambuliaji Habib Haji Kyombo ametoa tamko.
Starika huyo ambaye aliifunga Yanga mabao mawili mwezi uliopita kwanza amesema anashukuru Mwenyezi Mungu kumuwezesha kufanya vizuri pamoja na kupongeza kamati iliyomteua yeye kupata tuzo hiyo kwa kusema ni kama imemuongezea kasi.
Akifafanua zaidi kuhusu alichosema, alikuwa na haya ya kusema: "Hakika nashukuru Mungu kwa hiki alichonijaalia na namuonba anisaidie niweze kufanya vizuri katika michezo ijayo, kwani lengo langu ni kuwa mfungaji bora na kuisaidia timu yangu ya Mbao FC kufanya vizuri zaidi."
Akizungumza kwa njia ya Simu akiwa mkoani Mtwara wakijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Ndanda utaochezwa katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Jumamosi hii, Kyombo alisema alichofanya ni kama salamu kwa kuwa sasa anataka kuhakikisha anafunga ili awe mfungaji bora.
Kwa kauli hio, sasa anataka kushindana na Emmanuel Okwi wa Simba na Obrey Chirwa wa Yanga ambao ndiyo wamekuwa na kasi kubwa ya ufungaji msimu huu wa 2017/18.
Kwa sasa Kyombo anashika nafasi ya pili katika msimamo wa wafungaji bora ligi kuu akiwa amefunga mabao 7, akiwa nyuma ya Okwi mwenye mabao 8.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!