MBAO FC WAPIGWA NYUMBANI




Stand United imefanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhiai ya Mbao FC katika kipute cha Ligi Kuu ya Vodacom kilichochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, jana Jumamosi.
Mbao ambayo imekuwa ikizikomalia kwa nguvu Simba na Yanga hasa inapokuwa kwenye uwanja wake wa nyumbani, ilishindwa mikiki ya wapiga debe hao wa Shinyanga na kujikuta ikiruhusu bao hilo ambapo sasa Stand United imefikisha pointi 13.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Jacob Adongo aliyesaidiwa na Hellen Mduma na Martin Mwalyaje, bao la Stand United lilipatikana katika dakika ya 40 mfungaji akiwa ni mshambuliaji Vitalis Mayanga aliyefunga kwa penati baada ya kipa wa Mbao FC, Ivan Rugumandiye kumkamata miguu Landry Ndikumana ndani ya eneo la 18.
Kikosi cha Mbao FC kilikuwa; Ivan Rugumandiye, Vincent Philipo, Amos Abel, David Mwasa, Yusuph Ndikumana, Ibrahim Njohole/Ismail Ally dk75, James Msuva, George Sangija, Habib Kiyombo/Robert Ndaki dk81, Emmanuel Mvuyekure na Abubakar Mfaume/Abdul Segeja dk55.
Stand United; Mohamed Makaka, Makenzi Ramadhani, Miraj Maka, Ally Ally, Erick Mulilo, Ismail Gambo, Abdul Kassim, Bigirimana Babikakuhe, Abdallah Juma/Ally Khamisi dk75, Ndikumana Landry na Vitalis Mayanga.
Matokeo mengi ya ligi hiyo kwa jana Jumamosi
Mtibwa Sugar 0-0 na Njombe Mji FC (Uwanja wa Manungu).

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!