Posts

Showing posts with the label kandanda

YANGA WATINGA NUSU FAINALI FA, YAIPIGA ALLIANCE KIRUMBA

Image
KLAUS Kindoki leo amekuwa shujaa wa Yanga baada ya kuokoa penalti ya mwisho iliyopigwa na nahodha wa timu ya Alliance FC, Siraj Juma. Dakika 90 za mchezo wa leo wa hatua ya fainali ulikamilika kwa Alliance kutoshana nguvu na Yanga kwa kufungana bao 1-1. Yanga walitangulia kufunga bao dakika ya 38 lililofungwa na Heritier Makambo na kwa upande wa Alliance bao lilifungwa na Johson James. Klaus Kindoki Baada ya mwamuzi kuamua matuta, Yanga walianza kupiga kupitia beki kisiki Kelvin Yondani ambaye aligongesha kwenye mwamba, Paul Godfery alifunga penalti yake,Thaban Kamusoko alifunga kwa staili ya paneka, Mrisho Ngassa penalti yake iligonga mwamba na Haruna Moshi alifunga penalti kiufundi. Kwa upande wa Alliance penalti ya kwanza ilifungwa na Joseph John, Martin Kigi aligongesha kwenye mwamba, Dickson Ambundo alikosa penalti yake, Jofrey Luseke na Samir Vicent alifunga penalti. Baada ya kumaliza penalti 5 za awali kwa timu zote matokeo yalisoma 3-3 baada ya Yanga ku...

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Image
Mchezaji wa Zamani ambae aliisaidia Tanzania kuvuka katika hatua ya kushiriki michuano ya AFCON Mwaka 1979/80 na ndiye aliyeipatia Tanzania goli la Uhsindi, BENEDICT KINOPO, jana Ijumaa, Machi 22, 2019 alifika katika Uwanja wa Taifa na kuwapa hamasa vijana wanaoichezea timu hiyo ili washinde katika mechi ya Jumapili dhidi ya Uganda. Watanzania wanaimani na Timu ya Taifa kuwa itaibuka na ushindi katika mechi hiyo ambapo kuwa hamasa vimetenghenezwa ili Taifa stars kuona kama hawapo peke yao katika mbio hizo za kutaka kuvuka hatua hiyo. BAADA YA KUSHIRIKI HUU NDIYO ULIKUA MSIMAMO WA MATOKEO KWENYE KUNDI A, AMBALO TAIFA STARS ILIKUWA TAZAMA VIDEO AKIFUNGUKA

ALIYEWAUA YANGA ATANGAZWA KUWA MCHEZAJI BORA

Image
Mshambuliaji wa Mbao FC ya Mwanza, Habibu Kiyombo amechaguliwa Mchezaji Bora wa mwezi Disemba wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2017/2018. Kiyombo ameibuka mchezaji bora baada ya kuwashinda wachezaji wenzake wawili alioingia nao fainali kutokana na tathmini iliyofanywa na kikao cha Kamati ya Tuzo wiki hii. Kwa mwezi Disemba ambao timu 12 kati ya 16 zinazoshiriki ligi hiyo kila moja ilicheza mechi moja, Kiyombo aliisaidia timu yake kufunga mabao mawili katika mchezo dhidi ya Yanga ambao Mbao ilishinda mabao 2-0. Kutokana na matokeo hayo, Mbao ilipanda kutoka nafasi ya nane hadi ya saba katika msimamo wa ligi, huku Kiyombo akifikisha mabao saba ya kufunga kwake msimu huu, akiwa nyuma ya Emmanuel Okwi wa Simba anayeongoza akiwa na mabao nane. Kiyombo aliwashinda mshambuliaji wa Simba, John Bocco aliyefunga mabao mawili katika ushindi wa 2-0 wa Simba dhidi ya Ndanda na beki Bruce Kangwa aliyeisaidia Azam katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Stand United. Katika mchezo huo ...