Posts

Showing posts with the label home

MWAKINYO ATEMBELEA GLOBAL, ATAMBA HAJAONA WA KUPIGANA NAYE NCHINI

Image
Bondia Hassan Mwakinyo (kulia) akisalimiana na Meneja wa Global Group Abdallah Mrisho ofisini, Sinza Mori, Dar BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo, amesema kuwa hajaona bondia wa kupigana naye hapa nchini na jeuri hiyo anaipata kutokana na udhamini anaoupata kutoka Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya Michezo, SportPesa. Bondia Hassan Mwakinyo (Kulia) akisalimiana na Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally, leo Ofisi za Global Group zilizopo Sinza Mori, Dar. Kauli hiyo, aliitoa leo Jumanne mara baada ya kutembelea ofisi za Global Group inayochapisha magazeti ya  Championi, Spoti Xtra, Uwazi, Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Risasi Mchanganyiko, pamoja na vituo vya mtandaoni vya Global TV Online na +255 Global Radio,  Sinza-Mori jijini Dar es Salaam. Bondia Hassan Mwakinyo akifafanua jambo kitaalamu kwa Mhariri Mtendaji wa Global Group Saleh Ally. Mwakinyo, wikiendi iliyopita alifanikiwa kumpiga mpinzani wake Muargentina, Sergio Gonzalez ...

KAGERE, BOCCO WAMPA JEURI MBELGIJI KWA WAARABU

Image
K ASI  ya safu ya ushambuliaji ya Simba, imempa jeuri Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji, Patrick Aussems akitamka kuwa ana matumaini makubwa ya kuwafunga wapinzani wao JS Saoura nchini kwao Algeria. Simba inatarajiwa kuvaana na Saoura Machi 9, mwaka huu huko Algeria katika mchezo wa marudiano baada ya mchezo wa awali kushinda mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Safu ya ushambuliaji ya Simba inaongozwa na Mnyarwanda, Meddie Kagere, Emmanuel Okwi na John Bocco ambayo imefanikisha ushindi wa michezo minne migumu mfululizo dhidi ya Al Ahly 1-0, Yanga 1-0, African Lyon 3-0 na Azam FC 3-0. Akizungumza na  Championi Jumatatu,  Aussems alisema kuwa anafurahishwa na kasi hiyo ya ushambuliaji ambayo imeipa matokeo mazuri kutokana na kutimiza majukumu yao. Aussems alisema, bado anaendelea kuifanyia kazi safu hiyo ya ushambuliaji ili kuhakikisha wanaendelea na kasi hiyo ya kufunga kwenye michezo ijayo ya Ligi ya Mabingwa Afrika watakapokutana na Saour...

JOELLE BUKURU… MRUNDI WA SIMBA ANAYETAMANI KUICHEZEA TWIGA STARS

Image
LIGI ya Wanawake inazidi kuunguruma kwenye viwanja tofauti huku vipaji kibao vikishuhudiwa kutoka katika timu 12 zinazoshiriki ligi hiyo inayozaminiwa na kinywaji cha Serengeti Lite. Simba Queens ni miongoni mwa timu shiriki kunako ligi hiyo na tayari imeshashuka dimbani katika michezo mitano na kuvuna jumla ya pointi 13. Nyuma ya mafanikio hayo yupo mchezaji nyota wa Kikosi hicho, Joelle Bukuru ambaye anacheza nafasi ya kiungo mshambuliaji. Mrundi huyo huu ni msimu wake wa kwanza ndani ya ligi hiyo akiwa na jezi ya Simba. Amekuja nchini na mwenzake anayeitwa Aisha Djafar. Joelle Bukuru (kushoto mwenye mpira) akifanya yake. Bukuru ni miongoni mwa nyota ambao Jumapili iliyopita waliisaidia Simba kuibuka na ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Yanga Princess katika mwendelezo wa ligi hiyo, mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Karume, Dar. Championi Jumatano  limefanya mahojiano na nyota huyo juu ya maisha yake ya kwa jumla. “Naitwa Joelle Bukuru, nimezaliwa Burundi kati...

SIMBA KUSHUSHA MZIKI MNENE PEMBA

Image
Wachezaji wa timu ya Simba SC KAMA Azam walijua kwamba Simba itachezesha kikosi B kwenye fainali za Mapinduzi wamechemka. Simba inashusha mziki wote leo mjini Pemba. Katika mchezo huo Simba na Azam zitakuwa zinakutana kwa mara ya tatu fainali kwenye michuano hiyo ambapo mara ya kwanza zilikutana fainali mwaka 2012, 2017 na sasa 2019. Azam Fc ndiyo mabingwa watetezi wa kombe hilo wametwaa mara mbili mfululizo sasa. Meneja wa Simba, Abbas Ali alisema kuwa; “Baadhi ya wachezaji watatakiwa kwenda kuungana na wenzao kule Pemba na hii ni kutokana na kocha jinsi atakavyokuwa amepanga nani aende na nani abaki na lengo ni kupata matokeo.” Mudhathir Yahya wa Azam Fc, amesisitiza kuwa watapamba katika fainali dhidi ya Simba leo kwani anajua kwamba watapania na wakishinda watatamba sana. Yussuf Mlipili wa Simba alisema hawatowaangalia usoni Azam katika fainali ya leo kwani wanataka kuthibitisha kwamba wao ni imara na wana kikosi kipana.

AZAM FC MABINGWA MARA TATU MFULULIZO KOMBE LA MAPINDUZI

Image
Timu ya Azam FC wameifunga Simba SC kwa bao 2-1 kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, na kufanikiwa kutwaa Kombe la Mapinduzi kwa Mara ya 3 sasa. Wafungaji wa Azam ni Mudathir Yahya na  Obrey Chirwa ameifungia Azam FC bao la pili akimalizia kwa kichwa krosi ya Nickolas Wadada dakika ya 72. Bao la Simba lililofungwa na Yusuph Mlipili dakika ya 63.

SIMBA TISHIO CAF, WAIGONGA JS SAOURA BAO 3-0

Image
Kikosi cha timu ya Simba kilichoanza dhidi ya JS Saoura TIMU ya  Simba  wamefanikiwa kuwapa furaha mashabiki wao na  Watanzania  kwa Ujumla baada ya kuibuka na ushindi wa bao 3-0 dhidi ya timu ya  Jeunesse Sportive de la Saoura  maarufu kama  ‘JS Saouro’  kutoka nchini  Algeria. Kikosi cha JS Saoura kilichoanza dhidi ya Simba. Mchezo huo wa  Kundi D  wa  Ligi ya Mabingwa  barani  Afrika , umepigwa leo Jumamosi, Januari 12, katika Uwanja wa Taifa jijini  Dar es Salaam. Mshambuliaji Emmanuel Okwi ndiye alikuwa wa kwanza kuiandikia Simba bao la kuongoza dakika ya 45+2 kabla ya kwenda mapumziko baada ya kufanya shambulizi hatari na kuwahesabu mabeki wa JS Saoura. Simba waliokuwa wakishambulia muda wote wa mchezo huo, Meddie Kagere alifanikiwa kuiandikia Simba bao la pili 51 kisha kurudi tena nyavuni dakika 16 baadaye na kuiandikia tena bao la tatu dakika ya 67. Mpaka dakika 90 zinakwisha, Si...