SIMBA YAMTAMBULISHA RASMI 'MFARANSA' PIERRE LECHANTRE
Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, hii leo Ijumaa imemtambulisha rasmi kocha mkuu mpya wa timu hiyo, Pierre Lechantre amabye amechukua nafasi iliyoanchwa na Joseph Omog aliyetimuliwa hivi karibuni.
Kocha Pierre Lechantre ametambulishwa katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Serena jijini Dar tukio lililoendana na kusainishana mikataba.
Kocha huyo ametua nchini Tanzania akiwa pamoja na kocha wa viungo Amin Mohamed Habib ambapo kwa pamoja watafanya kazi na Masoud Djuma ambaye ndiyo yupo kikosini kwa sasa. Kocha Lechantre amewahi fundisha timu ya taifa ya Cameroon iliyochukua ubingwa wa Afrika.
Kikosi cha Simba chenyewe kipo mjini Bukoba kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Kagera Sugar utakaochezwa Jumatatu ijayo, hivyo, Lechantre ataanza kazi mara moja timu itakaporejea Jumanne baada ya mchezo huo.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara pia amewashukuru mashabiki wa Simba kwa sapoti ambayo wameionyesha wakati mchakato ulipokuwa ukiendelea.
Hii ni mara ya kwanza kwa kocha huyo raia wa Ufransa kufundisha timu ya Tanzania.
Akizungumza baada ya kusaini mkataba, Lechantre alisema: "Nitajitahidi kufanya kazi na kocha Djuma, kuipigania timu kuipeleka mbele katika mashindano ya Afrika.
"Nipo hapa kuipigania timu na kumfanya kila mtu awe na furaha katika klabu."
Katika mkutano huo Simba iliwatangaza viongozi walioteuliwa kuongoza kamati ya maadili itakayoongozwa na Mwenyekiti, Suleiman Kova aliyekua mkuu wa Polisi, Robert Selasela, Suleiman Ali aliyekua katibu wa zoezi la kuibadilsha Simba kuwa kampuni pamoja na Steven Ali.
Comments
Post a Comment