Posts

Showing posts with the label KIMATAIFA

La Galaxy Wampa Ninja Namba 51

Image
 BEKI wa zamani wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ juzi Ijumaa alitambulishwa rasmi katika mtandao wa klabu ya La Galaxy II kama mchezaji wa timu hiyo huku akiwa amepewa jezi namba 51. Ninja amejiunga na timu kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea katika timu ya MFK Vyskov ya Jamhuri ya Czech baada ya kumaliza mkataba wake wa miwili na Yanga akiwa ametokea Taifa Jang’ombe ya Zanzibar. Ninja alitambulishwa katika mtandao rasmi wa timu hiyo ambao unahusika kutoa taarifa za timu hiyo anayocheza mshambuliaji wa zamani wa Barcelona na Manchester United, Zlatan Ibrahimović. Akizungumza na mtandao huo, meneja mkuu wa timu hiyo, Dennis te Kloese alisema kuwa wamesaini beki huyo kutoka Tanzania kwa mkataba wa mkopo wa muda mrefu akitokea katika klabu ya MFK Vyskov huku akiwa tayari ameshapa kibali chake cha uhamisho wa kimataifa ITC na kibali cha kufanyia kazi nchini maarufu kama P1 Visa. “Tumemsajili Abdalla (Ninja) katika orodha ya wachezaji wetu kwa ajili msimu ujao...

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

Image
 NAHODHA wa timu ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’, Mbwana Samatta amefunga mabao matatu (hat-trick), katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza nchini Ubelgiji dhidi ya Waasland-Beveren. Samatta aliiongoza klabu ya KRC Genk kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 katika mchezo huo uliochezwa juzi, kwenye Uwanja wa Freethielstadion, mjini Beveren. Mshambuliaji huyo alifunga mabao hayo, dakika za 53, 66 na 86, huku bao jingine likifungwa na Joseph Paintsil dakika ya 21. Samatta anakuwa mshambuliaji wa tatu kufikisha mabao manne, baada ya kucheza michezo minne ya ligi hiyo msimu huu, wengine ni Dieumerci Mbokani wa Royal Antwerp na David Okereke wa Club Brugge. Huo ni mwanzo mzuri kwa Samatta ambaye msimu uliopita aliimaliza nafasi ya pili kwenye chati ya wafungaji bora wa ligi hiyo , akiwa na mabao 23, mabao mawili nyuma ya Hamdi Harbaoui wa Zulte Waregem aliyechukua kiatu cha ufungaji bora. Samatta sasa amefikisha mabao 66, katika mechi ya 160 za mashindano yote, t...

SIRI YA POGBA KUHAMA YAFICHUKA

Image
Paul Pogba WAKALA Mino Raiola imebainika ndio chanzo cha Paul Pogba cha kutaka kuondoka Manchester United. Staa wa zamani wa Tottenham na timu ya Taifa ya Misri, Ahmed Hossam `Mido’ alisema anafahamu kuwa wakala Raiola ndio anamvuruga Pogba kiasi cha kushikilia kutaka kuondoka msimu huu. Mido, ambaye alifanya kazi na Raiola kwa kipindi cha miaka 10, alisema anafahamu kuwa Raiola atakuwa bize akisaka timu ya kumnunua Pogba. Manchester United haina mpango wa kumuuza kiungo huyo ingawa kumekuwa na taarifa kuwa Pogba mwenyewe anashinikiza aondoke. Real Madrid kwa muda mrefu sasa inahusishwa kama timu ambayo inataka kumsajili Pogba na Mido amefichua kuwa wakala huyo atakuwa anafanya mambo yake chini kwa chini. “Wakala wa Pogba ni Mino Raiola na mimi nimefanya kazi na Mino, ambaye alikuwa wakala wangu kwa miaka 10 kwa hiyo nafahamu vizuri namna anavyofanya kazi,” alisema Mido. Mido alisema kuwa Raiola atakuwa ameshapiga hesabu zake na kuamini sasa ni wakati muafaka wa ...

AMUNIKE ATANGAZA CHA STARS AFCON

Image
Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kilichotangazwa na Kocha Emmanuel Amunike kwa ajili ya mashindano ya AFCON na CHAN.

OKWI AWEKA REKODI YA DAKIKA 270 SIMBA

Image
SIMBA ilicheza kwa dakika 270 katika Ligi ya Mabingwa ugenini hatua ya makundi bila ya kufunga bao lolote kabla ya straika Emmanuel Okwi, juzi kufunga katika robo fainali na kuweka rekodi ya kipekee. Okwi ameweka rekodi ya kuwa mfungaji pekee wa Simba ugenini kwenye mechi za tangu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya timu hiyo kucheza dakika 270, sawa na mechi tatu bila kufunga bao lolote. Mganda huyo alifunga bao hilo mbele ya TP Mazembe katika mechi ya pili ya robo fainali ya kombe hilo ambapo Simba walifungwa kwa mabao 4-1 na kutolewa. Kabla Okwi hajafunga, hakukuwa na mchezaji mwingine wa Simba ambaye alifunga bao kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ugenini tangu hatua ya makundi. Simba katika mechi zake za ugenini kuanzia hatua ya makundi, walicheza na Al Ahly wakafungwa 5-0, AS Vita 5-0 na JS Saoura 2-0.

TAIFA STARS VS SENEGAL, ALGERIA AFCON, MAKUNDI YAPO HAPA

Image
TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imepangwa Kundi C Kwenye michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon 2019) inayotarajiwa kuanza Juni 21 hadi Julai 19, mwaka huu. Droo ya makundi hayo ilichezeshwa jana usiku katika Mji wa Giza uliopo nchini Misri ambapo michuano hiyo ya 32 kwa mwaka huu inafanyika nchini humo. Katika kundi hilo, Taifa Stars imepangwa na Senegal, Algeria na Kenya, ambapo kwa mujibu wa ratiba ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf), Taifa Stars itaanza kucheza dhidi ya Senegal, kisha Algeria na kumaliza na Kenya. Hii ni mara ya pili kwa Taifa Stars kushiriki michuano hiyo, mara ya kwanza ilikuwa 1980 ambapo ilipangwa na timu za Guinea, Morocco na wenyeji Nigeria. Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia na Kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike, walikuwa miongoni mwa wageni waalikwa walioshuhudia tukio hilo la kupangwa makundi.

MAN CITY YAPIGWA NA SPURS UGENINI BAO 1-0

Image
TOTTENHAM Hotspur wakiwa kwenye uwanja wao mpya wa London, jana walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Man City kwenye kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Awali wengi waliamini kuwa Man City wana nafasi kubwa ya kushinda mchezo huu lakini mambo yakawa magumu kwao na kujikuta wakifungwa bao pekee katika dakika ya 78. Katika mchezo huo ambao kila timu ilitawala kwa wakati wake, Son alikuwa shujaa baada ya kuifungia Spurs bao hilo muhimu na likiwa ni la kwanza kwao la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye uwanja wao mpya. City walipata penalti ya utata mwanzoni tu mwa mchezo huo, lakini mshambuliaji wake Sergio kun Aguero shuti lake likapanguliwa na kipa wa Spurs, Hugo Lloris. Mwamuzi wa mchezo huo ilibidi atumie VAR kufahamu kama ni penalti au la baada ya Danny Rose kuunawa mpira kwenye eneo la hatari. Hata hivyo, baada ya penalti hiyo bado timu zote ziliendelea kushambuliana kwa zamu huku City wakikosa nafasi nyingi za wazi. T...

SIMBA KUWATOA KWAO TP MAZEMBE KAMA WAANGOLA

Image
KWA kiwango na takwimu za uwanjani walizoonyesha Simba jana dhidi ya TP Mazembe uwezekano upo wa kufuzu nusu fainali. Katika mechi hiyo ya kwanza ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba ilitawala kwenye umiliki wa mpira, pasi na kila kitu kama inavyoonekana kwenye jedwali. Lakini ukiachana na takwimu hizo, Mazembe waliingiwa hofu na matokeo hayo kutokana na takwimu za msimu uliopita ambapo walitoka suluhu na Agosto nchini Angola lakini wakaenda kutoa sare ya bao 1-1 Lubumbashi na kutolewa. Katika mechi ya jana, Mohammed Tshabalala wa Simba na Jackson Muleka wa Mazembe ndiyo wachezaji pekee walionyeshwa kadi za njano hadi kipindi cha kwanza kinamalizika. Tshabalala alimchezea vibaya Sissoko wakati Muleka alidanganya kuanguka ndani ya eneo la penalti katika mchezo huo ambao Paschal Wawa alitolewa dakika tatu za kwanza baada ya kuchezewa rafu na nafasi yake kuchukuliwa na Juuko Murshid. Simba walifanya shambulio moja kali la dakika ya 31 Kagere alipiga mpi...