MCHEZO WA MWADUI Vs NJOMBE MJI WASOGEZWA
Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limetangaza kuwa mchezo namba 114 kati ya Mwadui FC ya Shinyanga na Njombe Mji ya Njombe uliokuwa ufanyike Ijumaa Januari 26,
2018 imesogezwa kwa siku moja kupisha mazishi ya aliyekuwa kocha msaidizi wa Mwadui Jumanne Ntambi.
Mchezo huo sasa utachezwa Jumamosi, Januari 27, 2018.
Kocha huyo msaidizi wa Mwadui alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu kabla ya kufikwa na mauti.
Comments
Post a Comment