BOSI SIMBA SC ASHITAKIWA KWA KUGHUSHI NA UDANGANYIFU



SEKRETARIETI ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imemshitaki Msaidizi wa klabu ya Simba SC, Suleiman Kahumbu kwa tuhuma za kughushi na udanganyifu. 
Sekretarieti hiyo chini ya Kaimu Katibu Mkuu, Wilfred Kidau imewapeleka kwenye kamati ya Maadili viongozi wanne kwa kughushi na udanganyifu wa mapato kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya wenyeji, Ndanda FC na Simba SC ya Dar es Salaam uliochezwa Desemba 30, mwaka 2017 Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Taarifa ya TFF kwa vyombo vya Habari mapema leo, imesema kwamba wengine walioshtakiwa kwenye Kamati ya Maadili ni Msimamizi wa Kituo cha Mtwara, Dunstan Mkundi, Katibu wa Chama cha Soka Mtwara, Kizito Mbano na Katibu Msaidizi wa klabu ya Ndanda FC, Suleimai Kuchele. “Sekretarieti inawashtaki viongozi hao kwa makosa ya kughushi pamoja na udanganyifu wa mapato kwenye mchezo namba 94 kati ya Ndanda FC ya Mtwara dhidi ya Simba ya Dar es Salaam iliyochezwa Disemba 30, 2017 kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara,” imesema taarifa hiyo.
Kwa tuhuma hizo, viongozi hao watatakiwa kufika mbele ya Kamati Maadili iliyo chini ya Mwenyekiti Wakili Hamidu Mbwezeleni, Makamu wake, Wakili Steven Zangira, Wajumbe Glorious Luoga, Walter Lungu na Amin Bakhresa Januari 18, 2018.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!