RUVU SHOOTING 0-1 YANGA ‘LIVE’ FULL TIME, UWANJA WA TAIFA Harun Habari Za Kitaifa 21 January 2018 FacebookTwitter



FULL TIME
Dakika ya 95: Mchezo umemalizika, Yanga inapata ushindi wa bao 1-0, mfungaji ni Buswita.
Dakika ya 94: Yanga bado wanamiliki mpira muda mwingi.
Dakika ya 90: Zinaonyeshwa dakika tano za nyongeza.
Dakika ya 88: Juma Mahadhi anakosa nafasi ya wazi, akiwa yeye na lango anashindwa kuugusa mpira ujae wavuni.
Dakika ya 82: 84: Kasi ya mchezo imepungua kiasi.
Dakika ya 81: Ruvu wanamtoa Abdul Mussa anaingia Khamis Mcha.
Dakika ya 76: Issa Kanduru anapata kadi ya njano kw akumchezea faulo Hassan Kessy.
Dakika ya 71: Dante yuko chini baada ya kusukumwa na Kanduru.
Dakika ya 70: Pius Buswita anapewa kadi ya njano baada ya kuchomekea mguu Rajab Zahiri.
Dakika ya 68: Tambwe anatoka, nafasi yake inachukuliwa na Juma Mahadhi.
Dakika ya 67: Mwamuzi anatoa kadi kwa Damas Mwakwaya baada ya kumsukuma Ajibu na mashabiki Yanga kulalamika.
Fakika ya 66: Ajibu anapata kadi ya njano kwa kumsukuma beki wa Shooting.
Dakika ya 65: Issa Kanduru anakosa nafasi ya wazi akiwa karibu na lngo kabisa. 
Dakika ya 65: Inapigwa kona lakini wachezaji wa Yanga wanakosa umakini.
Dakika ya 65: Yanga wanafanya shambulizi kali, Kessy anahusika inakuwa kona.
Dakika ya 62: Tshishimbi anapigiana pasi na kipa wake.
Dakika ya 59: Ruvu wanafanya shambulizi kali.
Dakika ya 56: Andrew Vincent 'Dante' apata kadi ya njano kwa kucheza faulo.
Dakika ya 48: Yanga wanafika langoni mwa Ruvu lakini walinzi wanaokoa.
Dakika ya 45: Yanga wanaanza kwa kumiliki mpira.
Kipindi cha pili kimeanza.
MAPUMZIKO
Yanga wanaongoza bao 1-0
Yanga wanapata bao mfungaji ni Pius Buswita, anafunga kwa kichwa.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dakika ya 49: Yanga wanapata kona, Ajibu anapiga inaokolewa.
Dakika ya 48: Ruvu wanapiga pasi kadhaa, wanatawala mchezo, Shaban anabaki yeye na lango anapiga shuti linapaa juu ya lango.
Dakika ya 45: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 3 za nyongeza. 
Dakika ya 44: Mchezo umesimama kwa muda, Tambwe amemchezea faulo kipa wa Ruvu.
Dakika ya 40: Ayub wa Ruvu yupo chini ameumia, mwamuzi anazungumza na Kessy ambaye amemchezea faulo.
Dakika ya 35: Kasi ya Yanga siyo kubwa, Ruvu wanajibu mashambulizi kila Yanga wanaposhambulia.
Dakika ya 28: Kona inapigwa, Tambwe anapiga kichwa, almanurusa afunge.
Dakika ya 27: Kessy anapiga krosi, inaokolewa na beki wa Ruvu inakuwa kona.
Dakika ya 26: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Nkomola ambaye alionekana kuumia, anaingia Emmanuel Martine.
Dakika ya 25: Tambwe anaotea.
Dakika ya 23: Amiss Tambwe anachezewa faulo lakini mwamuzi anapeta.
Dakika ya 19: Nkomola ameumia anatibiwa kwa sekunde kadhaa kisha mchezo unaendelea. 
Dakika ya 17: Yanga wanashambulia, wanafanya shambulizi kali lakini mpira unaokolewa.
Dakika ya 15: Yanga wanapata faulo, straika wao Nkomola anachezewa faulo.
Dakika ya 14: Mchezo umebalansi.
Dakika ya 10: Ruvu wanalishambulia lango la Yanga lakini mpira unaokolewa.
Dakika ya 6: Yanga wanafika langoni mwa Ruvu lakini Ibrahim Ajibu anashindwa kumalizia kazi.
Dakika ya 5: Ruvu wanapata kona, inapigwa lakini inaokolewa.
Dakika ya 3: Timu zote bado zinasoma.
Mchezo umeanza.
Huu ni mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom unaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Ruvu Shooting ya Pwani inapigana na Yanga ya Dar es Salaam. 

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!