SIMBA 4-0 MAJIMAJI UWANJA WA TAIFA
FULL TIME
Dakika ya 94: Mwamuzi anamaliza mchezo, Simba inaibuka na ushindi wa mabao 4-0.
Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika nne za nyongeza.
Dakika ya 87: Majimaji wanapata nafasi lakini Six anashindwa kuitumia nafasi.
Dakika ya 84: Simba wanamtoa Kichuya, anaingia Laudit Mavugo.
Dakika ya 80: Bocco anawatoka walinzi wa Majimaji lakini shuti lake linapaa juu.
Dakika ya 79: Majimaji wanajaribu kujipanga lakini Simba wapo makini na wanaendelea kuwasumbua.
Dakika ya 70: Simba wanaendelea kutawala mchezo.
Dakika ya 68: Okwi anaipatia Simba bao la nne, anamalizia kazi nzuri ya John Bocco.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dakika ya 62: Simba wanapata faulo nje ya 18, inapigwa inatoka nje.
Dakika ya 50: Okwi anafunga bao la tatu kwa njia ya kichwa, aliunganisha mpira wa kona ulipigwa na Shiza Kichuya.
Dakika ya 49: Simba wanafanya shambulizi kali, Kapombe anafanya kazi nzuri lakini mpira unaokolewa.
Dakika ya 47: Marcel wa Majimaji anapiga shuti karibu na lango la Simba mpira unapaa juu ya lango.
Kipindi cha pili kimeanza.
MAPUMZIKO
Kipindi cha kwanza kimekamilika.
Dakika ya 48: Kichuya anafika langoni mwa Majimaji lakini kipa anauwahi mpira na kuudaka.
Dakika ya 45: Zinaongezwa dakika 3 za nyongeza.
Dakika ya 42: Simba wanamtoa Jamal Mwambeleko, anaingia Muzamiru Yasin.
Dakika ya 38: Shuti kali la Okwi linapanguliwa na kipa wa Majimaji.
Dakika ya 37: Majimaji wanafika tena langoni lakini wanakuwa wameotoa, mwamuzi anapuliza filimbi.
Dakika ya 35: Geofrey anapata mpira lakini anakuwa ameotea.
Dakika ya 31: Simba wanafanya shambulizi kali inakuwa kona.
Dakika ya 27: Straika wa Simba, John Bocco anaipatia timu yake bao la pili kwa njia ya kichwa akimalizia kazi nzuri ya Said Ndemla.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dakika ya 24: Bocco anapaisha mpira aliopewa na Shomari Kapombe. Bocco alibaki yeye na lango.
Dakika ya 22: Inapigwa faulo lakini inaokolewa.
Dakika ya 19: Mshambuliaji anafanyiwa faulo nje kidogo ya eneo la 18 lakini mwamuzi anapeta.
Dakika ya 16: Simba wanapata bao la kwanza mfungaji ni John Bocco, amefunga kwa kichwa.
Dakika ya 16: Simba wanaanza kujipanga na kulishambulia lango la Majimaji.
Dakika ya 11: Mambo bado hayajachanganya.
Dakika ya 7: Kasi ya mchezo haijawa kubwa.
Dakika ya 2: Majimaji wanafanya shambulizi kali langoni mwa Simba, kipa Aishi Manula anafanya kazi nzuri.
Huu ni mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kwenye Uwanja wa Taifa.
Comments
Post a Comment