HAYA NDO MANENO YA EMMANUEL OKWI

Image result for okwi simba sc

Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi ambaye amekuwa katika kiwango kizuri msimu huu wa 2017/18 amefunguka kuwa kipaumbele chake siyo kupata Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka bali ni kuisaidia Simba kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Okwi ambaye ni raia wa Uganda amesema nia yake ni kutaka kufunga kila mechi ili kuwa na mchango mkubwa ambao utaiwezesha timu hiyo kufikia malengo ya kushinda na kuwafurahisha mashabiki wao.
Mara ya mwisho Simba kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ilikuwa msimu wa 2010/2011, Okwi anaamini huu sasa ni msimu wao wa kufanya kweli na kurejesha furaha kwa Wanaasimba.
Hadi sasa Okwi anaongoza orodha ya wafungaji mabao katika ligi hiyo akiwa na mabao 10.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!