Posts

Showing posts from January, 2018

SIFA za kocha Mpya Wa SIMBA ( MFARANSA)

ALICHOKISEMA AMANI KYATA ANECHEZEA NAKURU STARS BAADA YA KUIFUNGA SIMBA

ELIAS MAGURI BADO AMEKWAMA KUJIUNGA NA POLOKWANE CITY YA AFRIKA KUSINI

Image
Mshambuliaji wa Mtanzania Elias Maguri ameendelea kuonekana katika mitaa ya Dar es Salaam baada ya dili lake kukwama kujiunga katika timu ya Polokwane City inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini. Awali ilielezwa kuwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba na Stand United aliyekuwa akicheza soka Uarabuni, alikuwa mbioni kujiunga na Yanga lakini mambo yakabadilika na akaelekea Afrika Kusini ikielezwa anaenda kujiunga katika timu ya Polokwane City. Maguri amesema ni kweli alishamalizana na Polokwane City kwa kuwa alishasaini mkataba wa awali kabla ya kwenda kushiriki katika michuano ya Kombe la Chalenji nchini Kenya lakini baadaye hawakukubaliana katika masuala ya maslahi. Amesema kuwa makato ambayo klabu hiyo iliyaibua katika dakika za mwisho ndiyo yalisababisha yeye kutosaini mkataba wa kuichezea timu hiyo. Kuhusu mipango yake, amesema anaendelea kusikilizia ofa kabla ya kuchukua maamuzi ya wapi pa kwenda.

AZAM FC UWANJANI LEO KUKIPIGA DHIDI YA SHUPAVU FC

Image
Kikosi cha Azam FC kiliwasili salama mkoani Morogoro kwa ajili ya kuvaana na Shupavu katika mchezo wa raundi ya tatu ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) utakaofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, leo Jumanne saa 8.00 mchana. Mara baada ya kuwasili jana mchana na kufikia katika Hoteli ya Oasis, kikosi hicho kilifanya mazoezi ya mwisho jana jioni kwenye uwanja huo utakaochezewa mechi, ambapo huenda benchi la ufundi likakifanyia mabadiliko madogo kikosi kitakachoanza kwa kuwapumzisha baadhi ya wachezaji. Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Nassor Cheche, amesema kuwa wanauchukulia uzito mchezo huo kwa kuhakikisha wanashinda kutokana na bingwa wa michuano hiyo kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika Kombe la Shirikisho Afrika (CC). “Kwa malengo hayo tumeuweka huu mchezo kwa kupambana kwa asilimia 100, na ndio maana toka vijana wetu wamemaliza mchezo uliopita dhidi ya Yanga wameendelea kukaa kambini ili kuhakikisha wapo salama na wanajiandaa tayari kupambana n...

YANGA YATUA MBEYA, KUKIPIGA LEO HII

Image
Kikosi cha Yanga kimewasili jijini Mbeya asubuhi ya leo kwa kwa ajili ya mchezo wao wa raundi ya tatu ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) dhidi ya Ihefu FC. Yanga iliondoka asubuhi ya leo kwa ndege kutoka Dar es Salaam ambapo ni saa chache kabla ya mchezo huo ambao utachezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini hapo. Mchezo huo utachezwa leo saa kumi jioni.

MANENO YA KOCHA MSAIDIZI WA KIKOSI CHA STAND UNITED KUHUSU KIFO CHA NTAMBI.

Image
Kocha msaidizi Wa kikosi cha Stand United ya mkoani Shinyanga Athumania Bilali (Bilo) amepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha aliyekua kocha msaidizi Wa kikosi cha Mwadui fc Jumanne Ntambi aliyefariki usiku wa tarehe 24 Januari mkoani Shinyanga. Akizungumza na Shutikali Kocha Bilali amesema ameumia sana na kifo cha Kocha Ntambi kwani amewahi kumfundisha katika timu ya Biashara Shinyanga Mnamo Mwaka 1992 "Hakika kifo cha Jumanne Ntambi kimesikitisha sana kwani alikua mwalimu Wangu katika timu ya Biashara Shinyanga pia ndiye aliyenishawishi Mimi kuingia katika kazi Hii ya ukocha" Akimuelezea kocha Ntambi Bilali amesema alikua ni Kocha Mwenye kujali kazi Yake na alikua ni Kocha aliyekua akiheshimu kila mtu hata kama amemzidi Mafanikio huku akiwataja nyota kadhaa waliopita kwenye mikono yake akiwemo Mshambuliaji wa zamani wa Kahama United Karume Songoro. Jumanne Ntambi alifariki Siku ya jumatano ya 25 saa Tatu za usiku akiwa mkoani Shinyanga na Mwili wake kusa...

MANARA ALICHOKISEMA BAADA YA USHINDI WA SIMBA SC JANA

Image
Simba ilipata ushindi wa mabao  4-0 dhidi ya Majimaji, jana Jumapili katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, baada ya ushindi huo kama kawaida Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alikuwa na jambo la kusema. Ikumbukwe kuwa katika ushindi huo mabao ya Simba yalifungwa na John Bocco na Emmanuel Okwi, kila mmoja alifunga mawili. Bocco ndiye ambaye alionyesha kiwango kizuri zaidi kwa kuwa pia alitengeneza bao moja la Okwi. Sasa kama kawaida yake Manara akayasema haya:  “Idadi ya magoli ya wahenga John Bocco na Emmanuel Okwi ni sawa na idadi ya magoli yote waliyofunga Gongowazi hadi sasa..nadhani sasa mtaelewa maana ya kikosi cha one B, goli 35.points 35 kisha unbeaten. Nisisahau, endeleeni pia kujiongopea eti mtatukuta, hivi Kwani zile mbeleko za jamaa yenu zipo safari hii?Shubamit!!!! “ Aidha, manara pia alitoa kauli hii: “Niseme nn zaidi ya kumshukuru Mungu..Alhamdulillah.....uzuri wake tunashinda kisha tunawapa burudani washabiki..wale walionuna Fansida 20 ukichang...

KOCHA AFUNGIWA, REFA ALIYECHEZESHA AZAM FC VS YANGA

Image
Maamuzi ya Kamati ya Bodi ya Ligi Kuu ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi kilichofanyika Januari 25, 2018 ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume,  Dar es Salaam. Mechi namba 95 (Mbeya City 1 vs Kagera Sugar 1). Klabu ya Mbeya City imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kutumia mlango usio rasmi kuingia uwanjani katika mechi hiyo iliyofanyika Januari 1, 2018 jijini Mbeya, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(14) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu. Kamati iliiagiza Sekretarieti ya Bodi ya Ligi kutoa waraka kwa wamiliki wa viwanja kuhakikisha timu zinaingia uwanjani kwa kutumia milango rasmi tu. Mechi namba 100 (Tanzania Prisons 3 vs Mbeya City 2). Kocha wa Mbeya City, Ramadhani Mwazurimo amefungiwa mechi mbili na kupigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano), adhabu ambayo imezingatia Kanuni ya 40(11) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Makocha. Kocha Mwazurimo...

SIMBA 4-0 MAJIMAJI UWANJA WA TAIFA

Image
FULL TIME Dakika ya 94: Mwamuzi anamaliza mchezo, Simba inaibuka na ushindi wa mabao 4-0. Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika nne za nyongeza. Dakika ya 87: Majimaji wanapata nafasi lakini Six anashindwa kuitumia nafasi. Dakika ya 84: Simba wanamtoa Kichuya, anaingia Laudit Mavugo. Dakika ya 80: Bocco anawatoka walinzi wa Majimaji lakini shuti lake linapaa juu. Dakika ya 79: Majimaji wanajaribu kujipanga lakini Simba wapo makini na wanaendelea kuwasumbua. Dakika ya 70: Simba wanaendelea kutawala mchezo. Dakika ya 68: Okwi anaipatia Simba bao la nne, anamalizia kazi nzuri ya John Bocco. GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO Dakika ya 62: Simba wanapata faulo nje ya 18, inapigwa inatoka nje. Dakika ya 50: Okwi anafunga bao la tatu kwa njia ya kichwa, aliunganisha mpira wa kona ulipigwa na Shiza Kichuya. Dakika ya 49: Simba wanafanya shambulizi kali, Kapombe anafanya kazi nzuri lakini mpira unaokolewa. Dakika ya 47: Marcel wa Majimaji anapiga shuti karib...

YALIYOANDIKWA KATIKA MAGAZETI YA MICHEZO LEO JUMAPILI, TAREHE 28.01.2018

Image

AZAM FC 1-2 YANGA SC

Image
Azam Wanatoka uwanjani vichwa chini MPIRA UMEKWISHA Dk 92, Chirwa anapiga krosi pale lakini inaokolewa  Dk 92, Juma Mahadhi anawekwa chini na inakua ni faulo DAKIKA ZA NYONGEZA Dk 90+3, Yanga wanapoteza nafasi pale baada ya Mwashiuya kupiga shuti lilitoka nje ya goli Dk 88, Kelvin Yondani yuko chini baada ya kuruka na kutua vibaya na mguu wake, anapewa huduma ya kwanza  DK 87, Salmin Hoza anapiga mpira na unakwenda nje bila madhara yoyote  Dk 85, Hassan Kessy anafanyiwa madhambi na unapigwa kuelekea Azam Dk 85, Mahundi anapiga faulo lakini inaokolewa na Yanga Dk 84, Himid Mao anawekwa chini na inakua faulo  Dk 81,  KADI NYEKUNDU    Salum Abubakar Salum anapewa kadi nyekundu kwa kumsukuma Hassan Kessy baada ya kuwa na kadi mbili za njano Dk 77,  KADI YA NJANO  nyingine inakwenda kwa Aggrey Moriss baada ya kucheza rafu Dk 76,  KADI YA NJANO   kwa  Kelvin Yondan anapewa na ni kadi ya...

MBAO FC WAPIGWA TENA NA RUVU SHOOTING

Image
Mabao mawili ya Khamis Mcha ‘Vialli’ jioni ya leo yametosha kuipa Ruvu Shooting ushindi wa 2-0 dhidi ya Mbao FC Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Mcha, kiungo mshambuliaji aliyeshinda taji la Ligi Kuu na Azam FC msimu wa 2013-2014, alifunga mabao yake katika dakika za 26 na 44. Na sasa Ruvu Shooting inafikisha pointi 14 na kupanda hadi nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu, baada ya kucheza mechi 15, wakati Mbao FC inabaki nafasi ya nane kwa pointi zake 15 za mechi 15. Mzunguko wa 15 wa Ligi Kuu utaendelea kesho kwa mechi nne; Mwadui FC watakuwa wenyeji wa Njombe Mji FC Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga, Azam FC wataikaribisha Yanga SC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, Mbeya City watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na Kagera Sugar wataialika Lipuli FC Uwanja wa Kaitaba, Bukoba. Duru la kwanza la Ligi Kuu litakamilishwa Jumapili kwa mechi mbili, vinara Simba SC wakimenyan...

HAYA NDO MANENO YA MAJIMAJI KUHUSU MECHI YAO NA SIMBA

Image
Kuelekea mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba dhidi ya Majimaji, Jumapili hii kuna tambo zimetolewa na straika wa Majimaji, Jerry Tegete. Jerry Tegete ambaye ni nyota wa zamani wa Yanga amedai kuwa timu yao ipo fiti kuelekea mchezo huo na kuwakumbusha Simba kuwa wenzao, Yanga waliponea chupuchupu wakati walipokutana na Majimaji katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma. Ikumbukwe kuwa Majimaji na Yanga zilitoka sare ya bao 1-1 ambapo Yanga ililazimika kutoka nyuma kupata sare hiyo. Simba kwa sasa ipo chini ya Kocha Mkuu mpya Pierre Lechantre raia wa Ufaransa ambaye anatarajiwa kukaa kwa mara kwanza kwenye benchi la timu hiyo katika mchezo huo wa Jumapili. Akizungumzia mchezo huo utakaichezwa kwenye Uwanja wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Tegete alisema kuwa ujio wa kocha huyo mpya hauwafanyi wao waogope na kupata matokeo mabaya, kwani wataingia uwanjani kwa ajili ya ushindi pekee. Tegete alisema, katika kuhakikisha timu yao inamaliza ...

WACHEZAJI WATATU WANAOWANIA TUZO MCHEZAJI BORA AZAM FC

Image
Wachezaji watatu wa Azam FC, kipa Razak Abalora, beki Bruce Kangwa na mshambuliaji Yahya Zayd, wamechaguliwa kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi wa NMB (NMB Player of the Month) Desemba-Januari. Tuzo hiyo inatolewa na wadhamini wakuu wa Azam FC, Benki ya NMB ambao wametoka kuongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja jana, ulioifanya kuendelea kuwadhamini mabingwa hao kwa msimu wa nne mfululizo tangu 2014/2015. Nyota hao wanaingia kwenye kinyang’anyiro hicho baada ya kufanya vizuri kwa miezi hiyo miwili, wakiiongoza Azam FC kutwaa taji la Kombe la Mapinduzi mwaka huu kwa mara ya pili mfululizo pamoja na kuisaidia katika mbio zake za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL). Tuzo hiyo itatolewa kwa mshindi Jumamosi hii wakati Azam FC ikivaana na Yanga kwenye mchezo wa ligi utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex saa 10.00 jioni. Mpaka sasa wachezaji watatu wameshaitwaa tokea ianzishwe msimu huu, ya kwanza akiibeba beki Yakubu Mohammed (Agosti-Septemba), mshambuliaj...

KAGERA SUGAR IMETOA MAAMUZI BAADA YA JUMA NYOSO KUMPIGA SHABIKI

Image
Wakati sakata la beki wa Kagera Sugar, Juma Nyoso kushikiliwa na Jeshi la Polisi la mkoani Kagera kutokana na kudaiwa kumshambulia shabiki na kusababisha apotezea fahamu kwa muda, kuna tamko limeolewa kutoka kwenye klabu yake. Ikumbukwe kuwa Nyoso anatuhumiwa kumshambulia shabiki huyo ambaye jina lake linatambulika kwa jina la Shabani Hussein tukio lililotokea muda mfupi baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Kagera Sugar dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera. Taarifa kutoka ndani ya Kagera Sugar zinaeleza kuwa uongozi wa klabu hiyo umeamua kutomchukulia hatua yoyote Nyoso ambaye aliachiwa Jumanne ya wiki hii kwa dhamana kutoka katika mikono ya jeshi la polisi. Kigogo mmoja wa Kagera Sugar amenukuliwa akisema kuwa suala hilo kwao litamalizwa ndani ya klabu kwa kuwa hawataki liwe la watu wote na hawana mpango wa kumchukulia hatua zozote za kinidhamu. Kwa kauli hiyo sasa Nyoso anasubiri mwendelezo wa pande mbili ambazo ni polisi kwa kuwa ni tukio lililoh...

MANENO YA KOCHA WA MAJIMAJI KUHUSU MECHI YA SIMBA NA MAJIMAJI ITAKAYOPIGWA WIKENDI HII KWENYE UWANJA WA TAIFA

Image
Kikosi cha Majimaji kinatarajiwa kjuwasili jijini Dar es Salaam, leo Alhamisi kwa ajili ya kuvaana na wapinzani wao, Simba katika pambano la Ligi Kuu ya Vodacom ambalo litapigwa wikiendi hii kwenye Uwanja wa Taifa. Ofisa Habari wa Majimaji, Onesmo Ndunguru ambaye timu yake inadhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya Sokabet amesema mipango yao ni kuwasili Dar Alhamisi hii wakiwa na kikosi kamili kwa ajili ya mchezo huo na Simba. Onesmo amesema wanatua Dar ili kupata pointi tatu kwa kuwa wanajua mchezo huo ni muhimu kwao. Alipoulizwa juu ya maandalizi yao kuelekea mchezo huo, Kocha wa Majimaji, Habib Kondo alisema: “Tunajua kwamba mchezo utakuwa mgumu ila tumejipanga vyema kwa ajili ya kupata pointi mbele ya wenzetu hao, tunakuja tukiwa kamili kwa maana ya kikosi chote na siku chache ambazo tutakaa huko zitatufanya kuzoea mazin­gira kabla ya kupambana na wapinzani wetu.”

MCHEZO WA MWADUI Vs NJOMBE MJI WASOGEZWA

Image
Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limetangaza kuwa mchezo namba 114 kati ya Mwadui FC ya Shinyanga na Njombe Mji ya Njombe uliokuwa ufanyike Ijumaa Januari 26, 2018 imesogezwa kwa siku moja kupisha mazishi ya aliyekuwa kocha msaidizi wa Mwadui Jumanne Ntambi.  Mchezo huo sasa utachezwa Jumamosi, Januari 27, 2018. Kocha huyo msaidizi wa Mwadui alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu kabla ya kufikwa na mauti.

CAF YATAJA WAAMUZI WATAKAOCHEZESHA MECHI YA YANGA Vs ST LOUIS FC LIGI YA MABINGWA

Image
Shirikisho la Mpira wa miguu Barani Africa (CAF) limetaja waamuzi watakaochezesha mchezo wa kwanza na mchezo wa pili wa Ligi ya mabingwa Africa kati ya Yanga ya Tanzania dhidi ya Saint Louis FC ya Seychelles. Mchezo wa kwanza utachezwa Februari 10, 2018 uwanja wa Taifa na utachezeshwa na waamuzi kutoka Ethiopia na Kamishna wa mchezo akitokea nchini Namibia. Mwamuzi wa kati atakuwa Belay Tadesse Asserese akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Tigle Gizaw Belachew na mwamuzi msaidizi namba mbili Kinfe Yilma Kinfe wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Amanuel Heleselass Worku na Kamishna Frans Vatileni Mbidi. Mechi ya pili itakayochezwa Seychelles kati ya Februari 20 na 21,2018 itachezeshwa na waamuzi kutoka Madagascar na kamishna atatoka Mauritius. Mwamuzi wa kati atakuwa Andofetra Avombitana Rakotojaona akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Lionel Hasinjarasoa Andrianantenaina na mwamuzi msaidizi namba mbili Pierre Jean Eric Andrivoavonjy na mwamuzi wa akiba Hamada el Moussa...

CAF WAIPA SIMBA WAAMUZI WA SUDAN KUSINI IKIPAMBANA NA GENDARMERIE

Image
Waamuzi kutoka Sudan Kusini wameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF kuchezesha mchezo wa kombe la Shirikisho kati ya Simba ya Tanzania na Gendarmerie Tnale ya Djobouti itakayochezwa Februari 21,2018 Uwanja wa Taifa. Mwamuzi wa kati atakuwa Alier Michael James akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Abdallah Suleiman Gassim ,mwamuzi msaidizi namba mbili Gasim Madir Dehiya wakati mwamuzi wa akiba akiwa ni Kalisto Gumesi Simon Samson na Kamishna wa mchezo huo kutoka Botswana ni Mmonwagotlhe Edwin Senai. Mchezo wa marudiano utakaochezwa Djibouti kati ya Februari 20 na 21,2018 wenyewe utachezeshwa na waamuzi kutoka Burundi na Kamishna wa mchezo atatokea nchini Rwanda. Mwamuzi wa kati ni Eric Manirakiza akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Pascal Ndimunzigo,mwamuzi msaidizi namba mbili Willy Habimana,mwamuzi wa akiba Pacifique Ndabihawenimana na kamishna Gaspard Kayijuka.

AZAM FC YATAMBA KUWA ITAISHANGAZA SIMBA KWA KUTWAA UBINGWA VPL

Image
Azam FC imeeleza kuwa ipo kwenye mbio za kimya kimya katika kuwania taji la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na kudai wataishangaza Simba kwa kutwaa ubingwa huo mwishoni mwa msimu huu 2017/2018. Hadi ligi hiyo ikiwa imemaliza raundi ya 14, Azam FC na Simba zimeonakana kuwa katika mbio kali za kuwania ubingwa wa ligi hiyo, matajiri hao wakishika nafasi ya pili kwenye msimamo wakiwa na pointi 30 wakizidiwa pointi mbili na Simba iliyokileleni baada ya kujikusanyia 32. Kauli hiyo imetolewa jana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Abdul Mohamed, wakati Azam FC ikiingia mkataba mpya wa mwaka mmoja na wadhamini wakuu Benki ya NMB na kuungwa mkono na Meneja wa timu, Phillip Alando. “Kwa sasa tuko katika mbio za kimyakimya, zisizo na tambo nyingi, tukiongozwa na dhamira ya dhati ya kutwaa taji hilo la ligi, tutalipa fadhila za kuaminiwa huku na NMB kwa kutwaa taji la VPL, kwa sababu Azam FC inaamini katika mafanikio kama kichocheo cha kuvutia wadhaamini wengine,” alisema Mohame...

HAYA NDO MANENO YA EMMANUEL OKWI

Image
Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi ambaye amekuwa katika kiwango kizuri msimu huu wa 2017/18 amefunguka kuwa kipaumbele chake siyo kupata Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka bali ni kuisaidia Simba kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom. Okwi ambaye ni raia wa Uganda amesema nia yake ni kutaka kufunga kila mechi ili kuwa na mchango mkubwa ambao utaiwezesha timu hiyo kufikia malengo ya kushinda na kuwafurahisha mashabiki wao. Mara ya mwisho Simba kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ilikuwa msimu wa 2010/2011, Okwi anaamini huu sasa ni msimu wao wa kufanya kweli na kurejesha furaha kwa Wanaasimba. Hadi sasa Okwi anaongoza orodha ya wafungaji mabao katika ligi hiyo akiwa na mabao 10.

KAGERA SUGAR 0-2 SIMBA ‘LIVE’ UWANJA WA KAITABA

Image
Mwamuzi anamaliza mchezo, Simba ikiwa ugenini inapata ushindi wa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Kaitaba, wafungaji ni Said Ndemla na John Bocco. Dakika ya 94: Okwi anakosa nafasi ya wazi hapa, kipa Juma Kasena anafanya kazi nzuri ya kuudaka mpira Dakika ya 90: Zimeshaongezeka dakika mbili, Simba wanapata kona. Dakika ya 89: Mashabiki wa Simba wanaongeza shangwe. Dakika ya 86: Straika wa Simba, Laudit Mavugo anapasha misuli, nje. Dakika ya 83: Mchezo umechangamka, kasi imeongezeka, Kagera wanafunguka, Simba nao wanapanda kushambulia. Dakika ya 79: John Bocco anaipatia Simba bao la pili akimalizia pasi nzuri ya Shomari Kapombe. GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO Dakika ya 74: Kagera wanapata faulo, inapigwa vizuri lakini Manula anadaka. Shangwe za Simba zinaongezeka. Dakika ya 70: Shomari Kapombe wa Simba anaingia, anatoka Gyan. Dakika ya 69: Said Ndemla anaipatia Simba bao la kwanza kwa shuti kali. GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO Dakika ya 65: Mchez...

JUMA NYOSSO NA JOHN BOCCO WAMEKUTANA LIVE LEO UWANJA WA KAITABA

Image
Simba wanatarajiwa kuwa wageni wa Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom, leo Jumatatu kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera. Katika mchezo huo SImba itakuwa ikiwania kurejea kileleni katika msimamo wakati Kagera Sugar ikipambana kukwepa kushuka daraja. Kocha Mecky Maxime ambaye ni bosi wa Kaggera Sugar amefunguka kuwa timu yake ipo swa kwa ajili ya mchezo huo akiwemo beki wake wa kati, Juma Nyosso. Ikumbukwe kuwa Juma Nyosso aliwahi kufungiwa kutocheza soka kwa miaka miwili kutokana na kumfanyia kitendo cha kidhalilishaji mshambuliaji John Bocco aliyekuwa Azam FC kipindi hicho. Nyosso atakuwa na kazi ngumu ya kuwadhibiti washambuliaji wa Simba akiwemo Bocco ambaye kwa sasa yupo Msimbazi wengine ni Emmanuel Okwi raia wa Uganda. Maxime amesema kikosi chake kipo fiti na wanachohitaji ni pointi tatu tu katika mchezo huo, huku akijinadi kuwa hawana hofu ya kuikabili Simba ambayo ndiyo kinara wa ligi kuu.

KAULI KUTOKA KWA MASOUD DJUMA KUHUSU KOCHA MFARANSA WA SIMBA

Image
Klabu ya Simba imemshusha nchini Kocha Pierre Lechantre raia wa Ufaransa kwa ajili ya kuinoa timu hiyo lakini kuna kauli kutoka kwa Masoud Djuma ambaye ndiye aliyekuwa akikaimu nafasi ya kocha mkuu klabuni hapo. Djuma alikuwa akiiongoza Simba kwa muda baada ya klabu hiyo kumtimua kazi Kocha Joseph Omog ambapo sasa imeshusha kocha mkongwe mwingine Pierre Lechantre ambaye ni raia wa Ufaransa. Kocha huyo Mfaransa ambaye ametua jijini Dar es Salaam akiwa na kocha wa mazoezi ya viungo, Mohammed Aymen Hbibi raia wa Morocco, kwa pamoja wamekaribishwa na ushindi wa mabao 4-0 wakati Simba ilipocheza dhidi ya Singida United. Akizungumzia ujio huo, Djuma ambaye ni raia wa Burundi alisema kwanza anamkaribisha sana na anampa maelezo yote juu ya timu tangu alipoikuta na mabadiliko aliyofanya. Alisema baada ya hapo iwapo ataamua kuendelea na mfumo wa sasa alioanzisha yeye ni sawa na kama ataamua kubadilisha na kuja na falsafa yake yote kwake ni sawa. "Mimi sina tatizo kabisa, namkar...

BOSI SIMBA SC ASHITAKIWA KWA KUGHUSHI NA UDANGANYIFU

Image
SEKRETARIETI ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imemshitaki Msaidizi wa klabu ya Simba SC, Suleiman Kahumbu kwa tuhuma za kughushi na udanganyifu.  Sekretarieti hiyo chini ya Kaimu Katibu Mkuu, Wilfred Kidau imewapeleka kwenye kamati ya Maadili viongozi wanne kwa kughushi na udanganyifu wa mapato kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya wenyeji, Ndanda FC na Simba SC ya Dar es Salaam uliochezwa Desemba 30, mwaka 2017 Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara. Taarifa ya TFF kwa vyombo vya Habari mapema leo, imesema kwamba wengine walioshtakiwa kwenye Kamati ya Maadili ni Msimamizi wa Kituo cha Mtwara, Dunstan Mkundi, Katibu wa Chama cha Soka Mtwara, Kizito Mbano na Katibu Msaidizi wa klabu ya Ndanda FC, Suleimai Kuchele.  “Sekretarieti inawashtaki viongozi hao kwa makosa ya kughushi pamoja na udanganyifu wa mapato kwenye mchezo namba 94 kati ya Ndanda FC ya Mtwara dhidi ya Simba ya Dar es Salaam iliyochezwa Disemba 30, 2017 kwenye Uwanja wa Nangwanda ...

MBAO FC WAPIGWA NYUMBANI

Image
Stand United imefanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhiai ya Mbao FC katika kipute cha Ligi Kuu ya Vodacom kilichochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, jana Jumamosi. Mbao ambayo imekuwa ikizikomalia kwa nguvu Simba na Yanga hasa inapokuwa kwenye uwanja wake wa nyumbani, ilishindwa mikiki ya wapiga debe hao wa Shinyanga na kujikuta ikiruhusu bao hilo ambapo sasa Stand United imefikisha pointi 13. Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Jacob Adongo aliyesaidiwa na Hellen Mduma na Martin Mwalyaje, bao la Stand United lilipatikana katika dakika ya 40 mfungaji akiwa ni mshambuliaji Vitalis Mayanga aliyefunga kwa penati baada ya kipa wa Mbao FC, Ivan Rugumandiye kumkamata miguu Landry Ndikumana ndani ya eneo la 18. Kikosi cha Mbao FC kilikuwa; Ivan Rugumandiye, Vincent Philipo, Amos Abel, David Mwasa, Yusuph Ndikumana, Ibrahim Njohole/Ismail Ally dk75, James Msuva, George Sangija, Habib Kiyombo/Robert Ndaki dk81, Emmanuel Mvuyekure na Abubakar Mfaume/Abdul Segeja dk5...

ADHABU YAIKWAMISHA YANGA KUTOMCHEZESHA KELVIN YONDANI LEO

Image
Beki wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani huenda ataikosa mechi ya leo dhidi ya Ruvu Shooting ya Ligi Kuu Bara itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yondani ataikosa mechi hii kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano alizozipata kwenye mechi zilizopita za ligi kuu. Kutokana na hali hiyo, timu inaweza kumtumia beki wa kati Nadir Haroub ‘Cannavaro’ au Said Makapu kucheza nafasi hiyo ya beki ya kati pamoja na Vicent Andrew ‘Dante’. Taarifa zinaeleza Benchi la Ufundi la Yanga tayari limeanza kuchukua tahadhari ya kuwaandaa baadhi ya wachezaji akiwemo Cannavaro atakayecheza nafasi ya Yondani. “Yondani ameondolewa kwenye mipango ya kocha katika kuelekea mechi dhidi ya Ruvu itakayochezwa keshokutwa leo Uwanja wa Taifa. “Beki huyo ataukosa mchezo huu kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano alizozipata katika michezo iliyopita ya ligi kuu,” alisema mtoa taarifa huyo. Meneja Mkuu wa Yanga, Hafidh Saleh alithibitisha Yondani kuondolewa kikosi...