SIMBA WATANGAZA BEI YA VIINGILIO KWENYE MECHI YA KESHO VS TANZANIA PRISON

Klabu ya soka ya simba kesho itashuka dimbani kukipiga dhidi ya maafande Wa Tanzania prisons katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara mchezo ambao utachezwa kwenye uwanja Wa Taifa jijini Dar es salaam.
Katika mchezo huo simba wanashukadimbani wakiwa na kumbukumbu ya kutwaa ubingwa Wa ngao ya hisani baada ya kuibanjua Mtibwa Sugar mabao 2-1mchezo uliounguruma kwenyeuwanja wa Ccm kirumba huko jijini Mwanza .
Afisa habari Wa klabu hiyo kongwe Haji manara ametangaza viingilio vya mchezo huo hii leo mbele ya waandishi Wa Habari huku kiingilio cha juu ikiwa elfu 15 kwa VIP A elfu 10 VIP B mzunguko ikiwa ni sh elfu 3 na watoto watapata fursa ya kuangalia mchezo huo kwa kulipia nusu ya kiingilio cha chini ya sh elfu 1500.
Pamoja na hayo manara amewataka mashabiki Wa simba kujitokeza kwa wingi uwanjani siku ya kesho Kama ilivyo kawaida kwa timu hiyo kujaza viwanja mbalimbali ambavyo wanacheza ilikuchagiza ushindi na kuuanza vyema msimu mpya wa ligi wa 2018/19.
” tumekuwa na tabia ya kuja kwa wingi viwanjani kwani inatia moyo, uongozi umefanya kazi kubwa ya kuandaa timu na sasa ipo tayari kwa mapanbano”alisema manara
Akizungumzia kuusu vibali vya wachezaji Deoglatus Munishi pamoja na Cletus Chama  manara amesema tayari Fifa wameshatoa maagizo kwa shirikisho la mpira wa miguu Zambia na Afrika ya kusini na hadi ifikapo augost 22 mwaka huu wachezaji hao wawe wameshapatiwa vibali vya kufanya kazi hapa nchini.


Ligi kuu soka Tanzania bara inatarajiwa kuanza kesho katika viwanja kadhaa huku changamoto kubwa ni kukoselana mdhamini mkuu atakaye simamia ligi hiyo.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!