HABARI ZA KIMATAIFABAADA YA KUWACHAPA ARSENAL, GUARDIOLA AANZA TAMBO


Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amesema klabu hiyo itaimarika hata zaidi kadiri siku zinavyosonga.
Alisema hiyo hata baada yao kuwazidi nguvu Arsenal mechi yao ya kwanza msimu huu Ligi Kuu England kwa kuwacharaza mabao 2-0, jana Jumapili.
Gunners walikuwa wanacheza mechi yao ya kwanza ya ushindani bila Arsene Wenger ambaye alikuwa amewaongoza tangu 1996 kabla ya kustaafu mwishoni mwa msimu uliopita.
Lakini hawakujiweza dhidi ya mabingwa hao watetezi kwenye Uwanja wa Emirates.
“Tuna wachezaji wengi sana ambao bado hawajafikia kiwango chao cha juu cha uchezaji lakini tumekuwa pamoja kwa misimu miwili na tunajua tunafaa kufanya nini,” alisema Guardiola na kuongeza:
“Tumecheza vyema sana kwa jumla na siku baada ya siku tutaendelea kuimarika na kuimarika.
“Nina furaha kuwa meneja wa Manchester City. Wamenipa kikosi kizuri sana. Siwezi kulalamika hata dakika moja.”

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!