KIMATAIFA MOURINHO AMTAJA ANAYESTAHILI KUPIGA PENATI KATI YA POGBA, SANCHEZ
Baada ya kudaiwa kuwa mastaa wawili wa Manchester United, Paul Pogba na Alexis Sanchez walivutana juu ya kupiga penati katika mchezo wao dhidi ya Leicester City, uamuzi umetolewa.
Wawili hao walionekana kuzungumza muda mfupi kabla ya Man United kupata penati hiyo kwenye Uwanja wa Old Trafford, Ijumaa iliyopita na ikaelezwa kuwa walikuwa wakibishana juu ya mpigaji.
Mourinho amesema: “Pogba ni mpigaji mzuri, anapenda majukumu hayo na ndiye chaguo la kwanza katika kupiga.
“Uwanjani kuna chaguo la pili na la tatu, hiyo inatokea ikiwa mmoja atakuwa hana hali ya kujiamini au hayupo tayari, lakini (Pogba) alikuwa tayari.”
Comments
Post a Comment