CRISTIANO RONALDO APEWA MWALIKO MAALUM REAL MADRID



Cristiano Ronaldo amepata mwaliko wa kurejea Real Madrid kwa ajili ya mchezo maalum wa kuthamini mchango wake kikosini hapo licha ya kuwa kwa sasa anaichezea Juventus ya Italia.
Mreno huyo ametua Juventus hivi karibuni kwa pauni 100m lakini amepewa mwaliko huo ambapo ni wa mwakani wakati wa mechi za maandalizi ya msimu (pre-season).
Uamuzi huo umechukuliwa na Rais wa Real Madrid, Florentino Perez ambapo utakuwa ni mwendelezo wa kuonyesha heshima kwa wachezaji walioifanyia makubwa Madrid, iliwahi kuwa hivyo kwa Raul, Iker Casillas pia alipewa mwaliko lakini ikashindikana kutokana na ratiba kumbana.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!