MDHAMINI MKUU WA LIGI KUU BARA KUTANGAZWA LEO
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Bodi ya Ligi (TPLB) imetoa taarifa kuwa kutakuwa na tamko rasmi kuhusu mdhamini mkuu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, Boniface Wambura, amesema mdhamini huyo watamtangaza leo Jumanne baada ya kufikia nao mwafaka.
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku chache zimepita TFF wakingie mkataba na Bank ya KCB ulio na thamani ya kiasi cha shilingi milioni 420 wakiwa kama wadhamini washiriki.
Wakati TFF wakisubiriwa kumtangaza mdhamini, pazia la michuano ya Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao litaanza Agosti 22 2018.
Comments
Post a Comment