HABARI ZA KITAIFAMANARA AFUNGUKA TIMU IPI INA MASHABIKI WENGI SIMBA, YANGA!
Mjadala wa timu ipi ambayo ina mashabiki wengi nchini Tanzania umeendelea kuwa gumzo kwa miaka mingi.
Hoja kubwa ni kati ya Simba na Yanga, ipo ambayo ni bora kuliko nyingine katika suala hilo la mashabiki.
Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara ameugusia mjadala huo kwa kutoa maoni yake:
Manara amesema haya: “Siku hizi sisikii zile lugha za walevi eti Yanga ndiyo team ya Serikali au kujiita team ya Wananchi!!, Nchi yetu Serikali haina team na Wananchi ni Watanzania wote!!”
“Taasisi zote rasmi na kwa vigezo vyovyote vile zimethibitisha pasi na roho mbaya kuwa Simba ndio klabu inayoongoza kwa kuwa na mashabiki wengi zaidi Tanzania.
“Anzia kwa kujaza viwanja kote nchini na hata dunia ya social media tumewacha maili milioni Gongowazi, Kiufupi haipo na haijaundwa any footboll club inayoweza kujaza umma huo kwenye friend match Afrika nzima, kabla ya kunitolea povu nipinge kwa data.”
Comments
Post a Comment