MARTIAL AMJIBU MAKAVU MOURINHO, AMWAMBIA FAMILIA KWANZA
Habari zilieleza kuwa Klabu ya Manchester United itampiga faini mshambuliaji wake raia wa Ufaransa, Anthony Martial baada ya kupewa ruhusa ya kuondoka kambini nchini Marekani kwenda kumjulia hali mkewe aliyekuwa anajifungia, kisha yeye kuzidisha muda wa ruhusa hiyo, sasa kuna mapya.
Anthony Martial mwenyewe amevunja ukimya kupitia ukurasa wake wa Twitter na kueleza lini atarudi.
Kocha Jose Mourinho alitarajia Martial angeenda mara moja na kurudi jana lakini imekuwa tofauti kwa mchezaji huyo, Martial licha ya tetesi zote ameandika hivi Twitter:
“Asanteni wote kwa jumbe zenu mlizonitumia mtoto wangu hajambo na mzima, kwa upande wa mama yake hali haikuwa nzuri kidogo lakini nashukuru Mungu hali yake imeimarika kwa sasa, samahani lakini familia yangu siku zote ndio kitu muhimu cha kwanza kuliko chochote, narudi kesho Manchester.”
Comments
Post a Comment