BOSI WA MBWANA SAMATTA AZUIWA KUINGIA DRC, KISA NI URAIS





Bosi wa zamani wa mshambuliaji Mbwana Samatta, Moise Katumbi ambaye aliondoka nchini DRC mnamo Mei 2016, siku moja baada ya kutolewa waranti ya kukamatwa kwake, amezuiliwa kurejea nchini humo.
Moise Katumbi ambaye ni kiongozi wa upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, amezuiwa kurudi nchini humo kugombea urais katika uchaguzi mkuu Desemba mwaka huu.
Serikali ya Congo imemzuia Gavana huyo zamani wa jimbo la Katanga anayeishi uhamishoni Afrika kusini kurudi nyumbani.
Kabla ya kuingia rasmi kwenye mchakato wa kuwania urais, Katumbi alipata umaarufu nchini Tanzania kutokana na kuwa ndiye mmiliki wa timu ya TP Mazembe ambayo ndiyo Mtanzania, Mbwana Samatta alikuwa akiichezea kabla ya kutimkia Genk ya Ubelgiji aliko hadi sasa.
Katumbi aliomba ruhusa kuingia nchini leo asubuhi kuwahi kuwasilisha makaratasi yake ya uteuzi wa chama kuwa mgombea urais kwa tume ya uchaguzi nchini.
Maafisa wa polisi huko Lubumbashi wameweka vizuizi katika bara bara kuu na usalama umeimarishwa ndani na katika maeneo yalio karibu na uwanja wa ndege.
Kuna mipango ya kuzifunga njia za ndege kutua kuizuia ndege ya Katumbi isitue DRC.
Bw Katumbi pia ni Rais wa klabu ya soka maarufu katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ya TP Mazembe.
Moise Katumbi ni nani?
Jina lake la mwisho pia Tshapwe
Anajulikana kama Moses Katumbi nchini Zambia, ambapo aliishi kwa miaka mingi
Tarehe ya kuzaliwa 28 Disemba 1964
Eneo la kuzaliwa ni Kashobwe
Ni kabila la Babemba
Ni kaka wa kambo wa Katebe Katoto, maarufu kama Rafael Soriano, na mfuasi wa Laurent Nkunda
Baba yake ni Padre Nissim Soriano, Mitaliano Myahudi kutoka Rhodes
Mama yake ni Virginie Katumbi, kutoka familia ya kifalme ya Kazembe
Rais wa kalbu ya Soka TP Mazembe Football iliopo Lubumbashi
Anajullikana kwa mapenzi yake na kofia za mtindo ‘Cowboy’
Waziri wa habari Lambert Mende anasema gavana huyo wa zamani kutoka jimbo lenye utajiri mkubwa wa madini atakamatwa iwapo atajaribu kuingia nchini kwa ndege ya usafiri wa abiria.
Katumbi aliondoka nchini Congo mnamo 2016 baada ya kukosana na rais Joseph Kabila.
Baadaye alishtakiwa kwa udanganyifu wa mali na alihukumiwa miaka mitatu gerezani pasi yeye kuwepo mahakamani.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!