Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Bodi ya Ligi (TPLB) imetoa taarifa kuwa kutakuwa na tamko rasmi kuhusu mdhamini mkuu wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, Boniface Wambura, amesema mdhamini huyo watamtangaza leo Jumanne baada ya kufikia nao mwafaka. Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku chache zimepita TFF wakingie mkataba na Bank ya KCB ulio na thamani ya kiasi cha shilingi milioni 420 wakiwa kama wadhamini washiriki. Wakati TFF wakisubiriwa kumtangaza mdhamini, pazia la michuano ya Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao litaanza Agosti 22 2018.




Habari ikufikie kuwa msafara wa timu ya Simba upo jijini Arusha kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Arusha United.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kesho Jumatano kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ikiwa ni maaluma baada ya Simba kupata mwaliko wa Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
Habari kutoka jijini hume zinaeleza kuwa msafara wa Simba umefikia Masailand Safari & Lodge.
Simba inajiandaa kwa ajili ya mchezo wa Ngao ya Jamii ambao utapigwa Jumamosi ijayo dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
Mtanange huo ni maaluma kwa ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2018/10.
Kwa sasa Simba ipo chini ya kocha Mbelgiji, Patrick J. Aussems.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!