HABARI ZA KITAIFA WACHEZAJI SITA WA SIMBA WAPIGWA CHINI TIMU YA TAIFA




Kocha mkuu Wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa stars Emanuel Amunike amewaondoa wachezaji sita (6)wa sambasc kwa kosa la kuchelewa kuingia kambini.
Akizungumza na waandishi Wa habari kwa niaba Ya Kocha huyo Katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini tff Wilfred Kidao amesema Kocha Amunike ameamua kuwaondoa kwenye kikosi chake wachezaji sita wa simba kutokana na utovu Wa nidhamu .
Kidao amesema Kama shirikisho lilifanya juhudi Ya kuzungumza na wachezaji na uongozi Wa simba ili kujua kikwazo kilocho sababisha wachezaji hao kushindwa kuripoti kambini ambapo mpaka Jana asubuhi ni mchezajin mmoja ambaye ni Aishi Manura.
Aidha kidao ameongeza kuwa mapendekezo Ya Kocha yalikuwa yanawahitaji wachezaji Wa simba na Azam fc kuripoti kambini jana kuanzia saa 12 asubuhi na mwisho wa kuripoti ni saa 6 usiku na hadi kufikia muda huo wachezaji wote wa azam walikuwa wamesha ingia kambini huku wa simba waliluwa bado hawajafika.
Wachezaji ambao wameenguliwa Katika timu ya taifa ni pamoja na Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Erasto Nyoni, Hasan Dilunga, John Bocco, na Shomary Kapombe.
Hatahivyo marabaada ya kuondolewa wachezaji hao kocha Amunike amewaita wachezaji wengine Saba ambao wataziba nafasi zilizo achwa na wachezaji wa wa simba ambapo wachezaji hao nipamoja na David Mwamtika na Frank Domayo kutoka azam fc Ally Abdulkadili na Poul Ngalema kutoka Lipuli fc Kelvin Sabato na Salumu Kihimbwa kutoka Mtibwa sugar na Salumu Kimenya kutoka Tanzania prisons.
Kutokana na suala hilo kidao ameahidi kuwachukulia hatua za kinidhamu ikiwemo kuwapeleka katika kamati ya utendaji Ya TFF kaimu Katibu mkuu Wa simba Hamisi Kisiwa meneja wa timu Robert Richard.
” Kocha amefungua milango kwa kila mchezaji anayetaka kucheza timu Ya taifa anachihitaji ni nidhamu “alisema kidao
Timu ya taifa imeingia kambini Jana katika hotel Ya sea scap iliyopo mikwecheni jijini dar es salaam kwa ajili Ya kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Africa dhidi Ya timu ya taifa ya Uganda mchezo ambao utachezwa septamber 8 mwaka huu jijini Kampala nchini Uganda

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!