LALIGA SASA KUCHEZWA MAREKANI NA CANADA



LaLiga imeingia mkataba wa miaka 15 na kampuni ya kimataifa ya michezo na burudani  iitwayo ‘Relevent’ ambayo inaonekana kutaka kuleta mechi ya ligi kuu ya Hispania kwa mara ya kwanza Amerika ya Kusini.
Tangazo la Alhamisi katika mtandao wa Twitter linaonesha mshirika wa LaLiga ‘Relevent, kampuni iliyoleta Kombe la Mabingwa wa Kimataifa (International Champions Cup) ina lengo la kukuza mchezo wa soka huko nchini Marekani na Canada.
Mtazamo wa ligi kuu za Ulaya kuwa mwenyeji katika sehemu nyingine za dunia sio jambo jipya, Ligi Kuu ya Uingereza ishawahi kujadili mwaka 2008 uwezekano wa kuwa na “michezo mingine katika mataifa mengine”, lakini majadiliano hayo hayakuzaa matunda.
Pamoja na ushirikiano hua wa LaLiga na  Amerika ya Kaskazini kuanzishwa, Mkataba huo unatarajiwa kukuza “soka la Hispania” katika nchi za Marekani na Canada kupitia watazamaji na wanunuaji bidhaa za makampuni yanayodhamini klabu hizo katika jezi, viatu na vifaa vingine vya michezo. Ushirikiano huo pia utaboresha maendeleo ya soka la vijana, makubaliano ya masoko, mechi za maonyesho na mipango ya kuwa na mechi rasmi ya LaLiga iliyofanyika Marekani.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!