KUHUSU MAN UNITED KUMCHUKUA ZIDANE TAMKO HILI HAPA…
Baada ya kuwa na habari kuwa Manchester United inamtaka Zinedine Zidane kuchukua nafasi ya Kocha Jose Mourinho, tamko limetolewa.
Klabu ya Manchester United imetoa tamko kuwa haina nafasi za kazi na kusisitiza, haijawahi kuwasiliana na Zidane ambaye ana umri wa miaka 46 na ni kocha wa zamani wa Real Madrid.
Baada ya kipigo cha mabao 3-2 ambacho walikipata Manchester United kutoka kwa Brighton, moto ukazidi kuwa mkali kuhusiana na nafasi ya Mourinho.
Chifu wa Man United, Ed Woodward ndiye aliyesema hawakufanya mazungumzo yoyote na Zidane kwa kuwa hawana nafasi ya kazi ya kocha mkuu kwa sasa.
Mourinho, 55, anaonekana yuko katika wakati mgumu katika kipindi hiki hasa kutokana na suala la Zidane kuendelea kuzungumzwa.
Huenda baada ya uongozi wa Manchester kuweka hadharani kwamba hauna mpango na Zidane, utapunguza presha kwa Mourinho lakini bado atatakiwa kukipa ushindi kikosi chake ili kufuta yanayoendelea.
Comments
Post a Comment