HABARI ZA KITAIFA ,YANGA UWANJANI BILA KOCHA MKUU KWENYE BENCHI DHIDI YA MTIBWA LEO
Kocha mkuu wa Yanga SC raia wa Kongo – DRC , ataendelea kuitazama timu yake ikicheza leo dhidi ya Mtibwa Sugar mechi yake ya kwanza ligi kuu akiwa Jukwaani huku msaidizi wake Mwandila akiongoza timu.Hii inatokana na kuchelewa kutoka kibali chake cha kufanya kazi nchini Tanzania ingawa tayari ana kibali cha ukazi. Uongozi wa Yanga umefuata taratibu zote za kumuombea vibali hivyo , kilichobaki na idara husika za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kukitoa kibali hicho cha pili baada ya taratibu husika kumalizika kufuatwa.
Comments
Post a Comment