MABOSI WA SIMBA WAPO CHIMBO WANASUKA MIKAKATI MIZITO



Kuelekea kuanza kwa msimu mpya wa 2018/19 uongozi wa Klabu ya Simba umeendelea kujiweka sawa kwa jili ya msimu huo.
Wakati uwanjani timu ikiendelea kufanya mazoezi kwa kasi kubwa, upande mwingine ni kuwa maandalizi ya kujiandaa kwa uongozi yameendelea chini ya Mohamed Dewji ‘Mo’ na Kaimu rais wa Klabu hiyo, Try Again.
Kikao cha Bodi ya Wakurugenzi kilichoongozwa na Mwekezaji Mohammed Dewji ‘Mo’ kilikuwa kilifanyika kujadili masuala mbalimbali ya klabu hiyo ambayo yatakuja kuwekwa hadharani baadaye.
Moja ya mikakati iliyojadiliwa kwenye kikao hicho ni pamoja na mbio za ubingwa kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara 2018/19.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema klabu imeamua kubadilisha mfumo huo kwa ajili ya kutomtegemea mtu mmoja na badala yake itakuwa na mwekezaji.
“Tumebadili muundo wa uendeshaji wa klabu ili kutomtegemea mfadhili, muundo huu unatupa fursa sisi na mwekezaji kuipeleke Simba mbele zaidi, shida ya kumtegemea mtu akisusa au vinginevyo ni shida”
“Sasa kikao cha Bodi ya Wakurugenzi Simba kinaendelea na lolote linaloamuliwa linafanywa na Bodi na si mtu” alisema.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!