HABARI ZA KITAIFAYANGA ITAYUMBA? SUBIRINI MTAONA MOTO WETU



Baadhi ya mashabiki wa soka wanaamini kuwa Yanga haipo vizuri na yawezekana ikawa na msimu mbaya lakini hilo linapingwa na beki wa timu hiyo.
Beki huyo ni Juma Abdul ambaye amekuwa klabuni hapo kwa miaka kadhaa tangu alipotua akitokea Mtibwa Sugar amesema anaamini bado wanayo nafasi ya kufanya vizuri.
Juma Abdul amesema kuwa anaamini Yanga bado ipo vizuri na inaweza kufanya vizuri kimataifa na ndani ya nchi pia.
Ikumbukwe kuwa Yanga itacheza dhidi ya USM Alger ya Algeria katika mchezo ujao wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Amesema kuwa wao wanaendelea na mazoezi ya msimu mpya na wapo vizuri.

Comments

Popular posts from this blog

Msimu Mpya: Samatta Afanya Maangamizi Ubelgiji

ALIYEIPELEKA TAIFA STARS AFCON 1980 AFUNGUKA WALIVYOPAMBANA – VIDEO

Simba Vs Azam: Mtakula za Kutosha!