JONAS MKUDE ATOA KAULI KUHUSU KOCHA WAO MPYA
Licha ya kuwa hadi sasa bado Simba haijapata ushindi katika michezo yake miwili iliyopita ya kirafiki kujiandaa kwa msimu mpya wa 2018/19, kiungo wa timu hiyo Jonas Mkude amesema mambo mazuri yanakuja.
Mkude amemzungumzia kocha wao, Patrick Aussems kwa kusema kuwa ni kocha wa kipekee.
Kiungo huyo mwenye miaka kadhaa ndani ya Simba amedai kuwa kocha wao huyo raia wa Ubelgiji, anawaruhusu nyota wake kufanya wanachoweza uwanjani ilimradi matokeo mazuri yapatikane.
“Huyu kocha ni tofauti na wengine kwani hana mambo mengi sana ya kutubana, huwa anatuambia tucheze tunavyoweza na kila mmoja aonyeshe ufundi wake pindi tunapokuwa kwenye eneo la wapinzani,” alisema Mkude.
Ameongeza kuwa anaamini kuna mazuri yanakuja chini ya kocha huyo mpya.
Comments
Post a Comment